Uncategorized

NELSON MANDELA NA CHUO KIKUU FUJIAN KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIWANDA

Written by mzalendo

 

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof.Maulilio Kipanyula (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian Prof. Wu Renhua (Kushoto) alipotembelea Maktaba ya taasisi hiyo leo Aprili 15,2024. Katikati ni Mkurugenzi wa Taaluma Chuo cha Fujian Prof. Fang Hui.

Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kushirikiana na Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian nchini China katika masuala ya kuendeleza teknolojia, ugunduzi ili kuvutia wawekezaji kutoka kwenye viwanda.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula Aprili 15, 2024 wakati ya hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano katika Kampasi ya Tengeru Arusha.

Prof. Maulilio ameeleza kuwa, ushirikiano huo utahusisha mambo mbalimbali ikiwemo  kutoa mafunzo ya pamoja, kubadilishana wataalamu na wanafunzi ili kuwajengea uwezo, kuandika miradi ya utafiti ili kuja na suluhisho la pamoja katika kutatua changamoto za jamii.

“Kupitia teknolojia zitakazozalishwa kwenye ushirikiano huu, zitatoa fursa za soko la pamoja katika viwanda vya ndani ya nchi na nchini China lengo ikiwa ni kutatua changamoto zinazoikabili jamii” anasema Prof. Maulilio.

Naye Prof. Wu Renhua Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian nchini China ameleza kuwa, makubaliano hayo ni hatua ya kuleta maendeleo baina ya vyuo hivyo viwili lengo ikiwa ni kutengeneza kitovu (Hub) katika masuala ya teknolojia kwa manufaa ya Afrika na China.

Wajumbe hao kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian walipata fursa ya kutembelea Maktaba, Kiwanda kidogo cha DDI, Kituo cha Kompyuta yenye Uwezo Mkubwa wa Kuchakata Taarifa (HPC) na kituo cha Atamizi (Incubation) kwa lengo la kujifunza na kuona utekelezaji wa unaofanywa na taasisi hiyo katika masuala ya Tafiti, Bunifu, Uhandisi, Sayansi na Teknolojia

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian Prof. Wu Renhua (Kulia) wakisaini mkataba makubaliano katika masuala ya Taaluma na Utafiti leo Aprili 15,2024.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof.Maulilio Kipanyula (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian Prof. Wu Renhua (Kushoto) alipotembelea Maktaba ya taasisi hiyo leo Aprili 15,2024. Katikati ni Mkurugenzi wa Taaluma Chuo cha Fujian Prof. Fang Hui.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (kulia) akitoa maelezo kuhusu kiwanda Kidogo cha DDI kwa wajumbe wa Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian leo Aprili 15,2024.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (wa pili kushoto) akielezea kuhusu Kituo Atamizi kwa watafiti na wabunifu wa ndani na nje ya taasisi kwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian Prof. Wu Renhua (wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Taaluma Chuo cha Fujian Prof. Fang Hui na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Bunifu Prof. Revocatus Machunda leo Aprili15,2024.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Fujian Prof. Wu Renhua (wa pili kushoto) na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Taaluma Prof. Fang Hui , kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Tafiti na Ubunifu Prof Anthony Mshandete na wa kwanza kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi Mipango,Fedha na Utawala Dkt. Dida Mussa pamoja na menejimenti ya Taasisi leo Aprili15,2024.

About the author

mzalendo