Featured Kitaifa

SHUWASA : TUNAENDELEA NA MATENGENEZO BOMBA LILILOPASUKA KWENYE MTO MHUMBU

Written by mzalendoeditor
Kaimu Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usimamizi wa Usafi SHUWASA, Mhandisi Uswege Musa akionesha eneo la matengenezo ya bomba la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu na kusababisha huduma ya maji kutopatikana katika kata ya Ibadakuli na Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeendelea kuwaomba radhi wateja wake zaidi ya 10,000 wa kata ya Ibadakuli na Kolandoto Manispaa ya Shinyanga baada ya bomba kubwa lenye upenyo wa milimita 700 kupasuka ndani ya mto Mhumbu uliofurika maji ambapo kutokana na jitihada zinazoendelea huduma itarejea muda wowote.
 
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika eneo la Mto Mhumbu leo Jumamosi Aprili 13,2024 kushuhudia juhudi zinazofanywa na SHUWASA kuhakikisha huduma ya maji inarejea kwenye maeneo yaliyoathirika, Kaimu Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usimamizi wa Usafi SHUWASA, Mhandisi Uswege Musa amesema SHUWASA inaomba radhi kwa changamoto hiyo iliyotokea kutokana na mazingira yaliyo nje ya uwezo wao.
 
“Tupo eneo la Mto Mhumbu kutatua changamoto ya kupasuka kwa bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 700 linalopeleka maji katika kata ya Kolandoto na Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga. Maeneo haya yamekosa huduma ya maji tangu Aprili 8,2024 hadi leo hii tunaendelea na matengenezo. Baada ya kutokea changamoto ya kupasuka kwa bomba tulitoa tangazo kwa wananchi wa maeneo husika waweze kuhifadhi maji na tulianza hatua ya kutatua changamoto hii siku ya Jumatano na mpaka leo tupo hapa tunaendelea na jitihada za kurudisha huduma ya maji”, amesema Mhandisi Musa.
“Siku ya kwanza Jumatano tulianza kazi kwa ufanisi mzuri kabisa hadi kufikia jioni tulikuwa tumekamisha kazi kwa asilimia 50 lakini baadae tulikutana na changamoto ya maji kutoka katika mto Mhumbu yalijaa hadi kwenye eneo tunalofanyia kazi, mto ulijaa na kusababisha mafundi kuondoa vifaa vya kazi eneo la matengenezo”,ameeleza.
Amebainisha kuwa, kutokana na jitihada wanazoendelea nazo matengenezo yatakamilika leo ili kurejesha huduma kwa wananchi hivyo kuwaomba wananchi waendelee kuwa watulivu wanapoendelea kurejesha huduma ya maji kwenye maeneo yaliyoathirika.

Matengenezo yakiendelea katika bomba kubwa la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga

“SHUWASA inafanya kazi usiku na mchana, tunatarajia siku ya leo tutakamilisha kazi hii kwa sababu leo kuna hali ya jua lakini kama hali ya hewa haitabadilika inaweza kutukwamisha kwa sababu changamoto kubwa iliyopo katika eneo la matengenezo ni kwamba kuna chemchemi kubwa kutokana na kwamba tupo katikati ya mto Mhumbu, kuna maji kutoka chini ya mto yanapenya kuja kwenye eneo la matengenezo ambayo inatuwia ugumu kwa kiasi flani kufanya matengenezo haya”,ameongeza Mhandisi huyo.
 
Kwa upande wake, Kaimu Meneja Uzalishaji na Usambazaji Maji SHUWASA, Mhandisi Salum Ramadhan Ndelema amesema bomba kubwa maji la milimita 700 lilipata majeraha tangu Aprili 8,2024 na kushindwa kuendelea kusukuma maji kuelekea kwa wateja wa Bugweto na Kolandoto hivyo ikawalazimu kufunga maji ili waweze kuziba jeraha hilo.
 
“Mpaka sasa hivi tunaendelea na kazi, na hii yote imesababishwa na hali ya mazingira ambayo haikuwa vizuri, hali ya mto kujaa maji mengi na kurudisha maji kwenye eneo ambalo tunafanyia kazi ya matengenezo. Tulitegemea kazi hii ingemalizika mapema lakini tunaendelea na mafundi wetu ili kuhakikisha tunarudisha huduma katika maeneo yaliyoathirika, sasa tunaelekea kukamilisha kazi hii kwa sababu sasa bomba linaonekana tofauti na hapo awali”,amesema Mhandisi Ndelema.
Kaimu Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usimamizi wa Usafi SHUWASA, Mhandisi Uswege Musa akielezea changamoto ya kupasuka kwa bomba la maji katika Mto Mhumbu na kusababisha huduma ya maji kutopatikana katika kata ya Ibadakuli na Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Mkurugenzi Usambazaji Maji na Usimamizi wa Usafi SHUWASA, Mhandisi Uswege Musa akionesha eneo la matengenezo ya bomba la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu na kusababisha huduma ya maji kutopatikana katika kata ya Ibadakuli na Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
 
Kaimu Meneja Uzalishaji na Usambazaji Maji SHUWASA, Mhandisi Salum Ramadhan Ndelema akielezea changamoto ya kupasuka kwa bomba la maji katika Mto Mhumbu na kusababisha huduma ya maji kutopatikana katika kata ya Ibadakuli na Kolandoto Manispaa ya Shinyanga
Matengenezo yakiendelea katika bomba kubwa la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga
Matengenezo yakiendelea katika bomba kubwa la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga
Matengenezo yakiendelea katika bomba kubwa la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga

Matengenezo yakiendelea katika bomba kubwa la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga

Matengenezo yakiendelea katika bomba kubwa la maji lililopasuka katika Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga

Muonekano wa sehemu ya Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga mahali panapopita bomba la maji ya SHUWASA
Muonekano wa sehemu ya Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga mahali panapopita bomba la maji ya SHUWASA
Muonekano wa sehemu ya Mto Mhumbu Manispaa ya Shinyanga mahali panapopita bomba la maji ya SHUWASA

About the author

mzalendoeditor