Featured Kitaifa

MAAFISA WA UHAMIAJI SHINYANGA WAPANDA MITI KWENYE MAKAZI YA ASKARI, WATOA MISAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM BUHANGIJA

Written by mzalendoeditor
Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura akimwagilia mti maji katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wamepanda miti katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga pamoja na kutoa misaada mbalimbali ikiwemo chakula, taulo za kike na TV ya Inch 75 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Jumuishi kilichopo Mjini Shinyanga.
 
Maafisa hao wa uhamiaji wakiongozwa na Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura aliyeambatana na Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku wamefanya zoezi la upandaji miti na kutoa misaada katika Kituo cha kulelea watoto cha Buhangija leo Jumamosi Machi 23,2024.
 
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura amesema wamepanda miti 100 katika eneo la makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga.

“Tumekutana leo hapa katika makazi ya askari sehemu ya Ibinzamata kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Kamishina Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala ambaye alituagiza tupande miti ili kutunza mazingira pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Tumepanda miti 100 katika eneo la ndani pamoja na eneo la nje linalozunguka makazi”,amesema ACI Kajura.
 
Amesema zoezi la upandaji miti litakuwa endelevu na kwamba watapanda miti katika taasisi na shule kadri watakavyoweza ili kuendelea kutunza mazingira huku akiwasihi askari hao kuitunza na kuilindi ikue ili kufikia lengo ambalo serikali inakusudia katika kutunza mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
 
Katika hatua nyingine amesema katika kipindi hiki cha Mfungo wa Kwaresma na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wamefika katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu Buhangija Jumuishi katika Manispaa ya Shinyanga na kutoa msaada wa chakula ikiwemo unga na mchele na juisi lakini pia TV kubwa ya Inch 75 itakayosaidia watoto hao kujifunza masomo yao.
 
“Tumekuja katika kituo hiki kwa ajili ya kutoa sadaka yetu, tumebatika kuleta baadhi ya mahitaji ikiwemo Tv ambayo itasaidia watoto kujifunza, kuongeza umakini na usikivu wa uelewa katika masomo yao”,amesema.
 
Naye Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku amesema lengo la maafisa wa Uhamiaji kufika katika kituo cha Buhangija Jumuishi pia ni moja ya shughuli walizokuwa wamepanga kufanya Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
“Sisi kama Chombo cha Ulinzi na Usalama tumewiwa kuja kutoa msaada katika Kituo cha Buhangija kwa sababu sisi pia ni wazazi, tuna watoto. Tumekuja angalau tufanye chochote kwa ajili ya watoto, japokuwa hatuwezi kutatua changamoto zenu zote lakini pale tulipoguswa tumekileta”,amesema SI. Lydia.
 
Kwa upande wake Mwalimu Mlezi wa watoto katika kituo cha Buhangija Mashinde Elias amewashukuru maafisa wa uhamia kufika katika kituo cha Buhangija na kuwapatia msaada na kuwaomba wadau kuendelea kufika katika kituo ambacho kinalea watoto ualbino, viziwi na wasioona.
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wakiwa wameshikilia miche ya miti kwa ajili ya kupanda katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Machi 23,2024  – Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura akizungumza wakati Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wakipanda miti katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga
Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura akipanda mti katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga
Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura akiweka udongo kwenye shimo la mti aliopanda katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga
Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura akimwagilia mti maji katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku akipanda mti katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku akimwagilia mti maji aliopanda katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la upandaji miti likiendelea katika makazi ya askari wa Uhamiaji Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga

Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura akizungumza katika Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga wakati Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wakitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku akizungumza katika Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Manispaa ya Shinyanga wakati Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wakitoa misaada mbalimbali ya kibinadamu

Misaada mbalimbali ya kibinadamu iliyotolewa na Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga
Misaada mbalimbali ya kibinadamu iliyotolewa na Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija

Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura na Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku (kulia) wakikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo TV yenye Inch 75 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija Manispaa ya Shinyanga

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga SI. Lydia Angumbwike Mwamsiku (kulia) akikabidhi taulo za kike katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija Manispaa ya Shinyanga

Kamishna Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga ACI. Emmanuel Kajura (kulia) akikabidhi chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum Buhangija Manispaa ya Shinyanga
Mwalimu Mlezi wa watoto katika kituo cha Buhangija Mashinde Elias akitoa neno la shukrani

Watoto katika kituo cha Buhangija wakitoa neno la shukrani
Maafisa Uhamiaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu na watoto katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Jumuishi kilichopo Mjini Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendoeditor