Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE TAMISEMI YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MITATU TANGA

Written by mzalendo

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe Denis Londo imetembelea na kukagua miradi mitatu katika Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Miradi hiyo ni ujenzi wa nyumba ya viongozi wa kitaifa (Rest House), Shule ya Sekondari ya Kiomani iliyojengwa kwa mradi wa SEQUIP pamoja na ujenzi wa Barabara ya Kange yenye urefu wa km 2.3 kiwango cha lami nyepesi.

Katika ziara hiyo kamati imeambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi.

About the author

mzalendo