Featured Kitaifa

WABUNGE WA CCM ZANZIBAR WATOA MKONO WA POLE KWA RAIS WA ZANZIBAR DK. MWINYI

Written by mzalendo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Mbunge wa Jimbo la Pangawe Mhe.Haji Amour Haji akizungumza kwa niaba na kutowa mkono wa pole kwa Rais wa Zanzibar na Familia, kwa kufiwa na Baba yao Mzazi Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar,8-3-2024.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Haji Amour Haji Mbunge wa Jimbo la Pangawe Zanzibar (kushoto kwa Rais) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa kutowa mkono wa Pole kwa Rais wa Zanzibar na Familia, kwa kufiwa na Baba yao Mzazi Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendo