Featured Kitaifa

EWURA YAJIPANGA KUMTUA MWANAMKE KUNI NA MKAA KICHWANI

Written by mzalendo

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Machi 9,2024 jijini Dodoma katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani)  leo Machi 9,2024 jijini Dodoma katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza  katika banda la Mamlaka hiyo leo Machi 9,2024 jijini Dodoma kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.

EWURA YASHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE LA KUGAWA MITAJI NA VITENDEA KAZI VYA NISHATI SAFI YA KUPIKIA
EWURA YAJIPANGA KUMTUA MWANAMKE KUNI NA MKAA KICHWANI
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,amesema mamlaka hiyo ina wajibu kuhakikisha wanamtua Mwanamke kuni na Mkaa kichwani kwa kuhakikisha wanatoa leseni kwa wakati kwa wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza katika nishati safi ya kupikia.
Dkt. Andilile ameyasema hayo leo Machi 9,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.
Amesema taifa bado linatumia nishati isiyosafi kwa kupikia hivyo EWURA itahakikisha ina wajibu wa kuhakikisha inatekeleza mikataba ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ikiwemo uharibifu wa mazingira na madhara ya afya yanayosababidhwa na moshi wakati wa matumizi ya kuni na mkaa.
“EWURA tutahakikiha tunahamasisha uwekezaji katika nishati safi kwa kutoa leseni kwa wawekezaji kwa wakati ili wawekeze katika eneo hilo, pia tunaangalia upatikanaji wake katika maeneo mengi kwa kuangalia mwenendo wa bei za bidhaa hiyo,” amesema Dkt. Andilile.
Ameongeza kuwa:”Sisi kama EWURA tutahakikisha kama ilivyo dhamira ya Rais kumtua ndoo mama kichwani, tutamtua mwanamke kuni kichwani kwa kuhakikisha anatumia nishati ambayo itamrahisishia kupata maendeleo badala ya kuhangaika na nishati chafu ya kupikia,”.

About the author

mzalendo