Uncategorized

WAZIRI JAFO:SJMT,SMZ ZIMESAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO NYINGI ZA MUUNGANO

Written by mzalendo

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Najma Murtaza Giga bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Mbunge wa Madaba na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo Februari 09, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akishiriki kikao cha Bunge jijini Dodoma leo Februari 09, 2024.

…………………..

Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto nyingi za Muungano. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo bungeni jijini Dodoma Februari 09, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Najma Murtaza Giga aliyetaka kujua mikakati ya Serikali ya kuhakikisha changamoto za Muungano ambazo hazijapatiwa ufumbuzi hazileti madhara nchini na lini zitapatiwa ufumbuzi.

Akiendelea kujibu swali hilo, Dkt. Jafo amesema kuwa SJMT na SMZ zimetengeneza utaratibu wa kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za Muungano kupitia vikao vyake.

 

Amesema kuwa Serikali hizo mbili ziliunda Kamati ya Pamoja ya kutatua changamoto za Muungano ambayo huundwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za Muungano.

Waziri Jafo amefafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa Kamati ya Pamoja mwaka 2006 hoja 25 zimejadiliwa na kati ya hizo 22 tayari zimepatiwa na kuondolewa kwenye hoja za Muungano.

Halikadhalika, ameongeza kuwa hoja mbili zilizobaki katika orodha hiyo zipo katika hatua za kupatiwa ufumbuzi kupitia kamati hiyo inayoundwa na wajumbe kutoka SJMT na SMZ.

Aidha, Waziri Dkt. Jafo amesisitiza kuwa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali inayoongozwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wana nia ya dhati ya kuzitafutia ufumbuzi hoja hizo mbili zilizobaki.

Kwa upande Mhe. Giga ametoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutatua changamoto za Muungano na kuonesha imani kuwa zilizobaki zitatafutiwa.

About the author

mzalendo