Na Paul Mabeja, DODOMA

MBUNGE wa viti maalum Stella Ikupa, ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watu wenye ualibino mkoani hapa ikiwemo mafuta maalum ya kuwalinda na mionzi ya jua inayosababisha saratani ya ngozi.

Ikupa, alikabidhi msaada huo jana jijini hapa kwa Mkurugenzi wa Shirika linalijihusisha na masuala ya watu wenye ulemavu la Foundation For Disabilities Hope, (FDH) Maiko Salali.

“Leo nimekuja hapa kukabidhi msaada huu kwa watu wenye ulemavu vitu hivi ni mafuta maalum kwa watu wenye ualibino, kofia pamoja na miwani ambavyo vitawasaidi kujilinda na mionzi ya jua na kuondokana na tatizo la saratani ya ngozi”alisema Ikupa

Alisema, vifaa hivyo kwa watu wenye ualibino ni muhimu sana katika kulinda afya zao hivyo wadau wanapaswa kujiwekea utaratibu wa kusaidia kundi hilo mara kwa mara.

“Hivi vitu kwa watu wenye ulemavu ni kama chakula kwao watu mara nyingi wamekuwa wakihoji kwanini msaada kila siku lakini sisi watu wenye ulemavu vifaa hivi ni kama chakula kwetu hivyo msaada kama huu ni wa muhimu kwetu”alisema Ikupa

Ikupa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Ikupa Trust Fund, alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kusaidia makundi ya watu wenye uhitaji wakiwemo walemavu ambao wamekuwa na mahitaji mengi.

Kadhalika, aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuwezesha makundi ya watu wenye ulemavu.

Alisema, serikali imekuwa mstari wa mbele kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu nchini ikiwemo kuboresha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.

“Hivi karibuni bungeni kupitia swali langu serikali ilieleza kuwa ipo kwenye mchakato wa kuchambua takwimu za watu wenye ulemavu kupitia sensa ya watu na makazi iliyofanyika 2022 ili kupata idadi kamili itakayowezesha serikali kuhudumia kundi hilo kikamilifu”alisema

Naye, Mkurunzi wa FDH, Maiko Salali alisema wanamshukuru mbunge huyo kwa msaada wa vifaa hivyo ambao vitakwenda kuwasaidia watu wenye ualibino mkoani hapa.

“Tunamshukuru sana mweshimiwa Ikupa kwa msaada huu na kwa namna amabavyo amekuwa mstari wa mbele kusaidia watu wenye ulemavu na tunaahidi vifaa hivi vitawafikia walengwa wenye uhitaji katika maeneo mbalimbali mkoani hapa”alisema Salali

Previous articleJINSI NILIVYOMPONYA MPENZI WANGU UGONJWA WA KISUKARI! 
Next articleDKT.TULIA AKIFUNGUA MKUTANO WA KIBUNGE MAREKANI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here