Kitaifa

WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUTAKA KUIBA MAFUTA

Written by mzalendo

Na. OMAR HASSAN/ SAID BAKARI – ZANZIBAR.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kula njama na kutaka kuiba mafuta kwenye magari ya Miradi ya ujenzi wa barabara katika bandari ya Mwangapwani.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP DANIEL SHILA alisema Febuari, 02, 2024 majira ya saa tatu usiku huko eneo la Kitope kwenye maegesho ya magari ya Kampuni ya ORKUN, Jeshi la Polisi liliwakamata YOHANA KIFUTU CHAMBATI (31) mkazi wa Kitope na FATMA SAID HABIB (30) mkazi wa Kinyasini kwa kupatikana wakiwa na madumu na mipira ya kunyonyea mafuta kwa nia ya kutaka kuiba mafuta.

Aidha, katika tukio jengine Febuari, 04, 2024 majira ya saa nane na nusu mchana huko Kidoti Bwereu katika Wilaya ya Kaskakazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja, Jeshi hilo limemkamata YUSSUF RAMADHAN KHAMIS (24) mkazi wa Mikunguni Mkoa wa Mjini Magharib kwa tuhuma za wizi wa Pikipiki mbili.

Wakati huo huo Kamanda SHILA alikagua utendaji kazi wa Askari Polisi katika Mkoa huo na kuwataka Mafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi hilo kufanya kazi na kuzingatia Nidhamu, Haki, Weledi na Uwadilifu.

About the author

mzalendo