NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Igongwi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe unaolenga kutatua tatizo la maji kwa wakazi 9,717 waishio kwenye Vijiji vya Kitulila, Madobole, Luponde na Njoomlole.

Mhandisi Mahundi ameyasema hayo leo Februari 2 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Neema Mgaya aliyetaka kujua ni lini Mradi wa Maji wa Igongwi utakamilika katika Tarafa ya Igominyi Wilayani
Njombe.

Mahundi amesema hadi sasa utekelezaji
wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 78 na Serikali katika mradi huo tayari imekamilisha ujenzi wa vyanzo vinne vya
maji (Water Intakes), uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba kuu umbali wa Kilometa 49.77, ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa Kilometa 26 kati ya 35.6, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 32 kati ya 55, ujenzi wa matenki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 100,000.

“Kati ya matenki 4 pamoja na ujenzi wa miundombinu Sita (6) ya mfano ya kuvuna maji ya mvua iliyojengwa katika Shule za Msingi Madobole na Kitulila,Ofisi ya Serikali ya Kijiji Madobole na Zahanati ya Kijiji cha Kitulila. Kazi zote zilizosalia zinatarajiwa kukamilika kabla au ifikapo Mwezi Juni, 2024″amesema Mahundi

Previous article𝗛𝗔𝗜𝗝𝗔𝗪𝗔𝗛𝗜 𝗞𝗨𝗧𝗢𝗞𝗘𝗔, TANZANIA YAPATA UWEKEZAJI WA SHILINGI TRILIONI 4 NDANI YA MIEZI MITATU
Next articleSWEDEN KUSAIDIA UTEKELEZAJI WA MRADI WA SGR NA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) DAR ES SALAAM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here