Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, walipokutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden, ikiwa na ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden mwezi Septemba, 2023.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden, ikiwa na ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden mwezi Septemba, 2023. Kulia ni Balozi wa Biashara Endelevu-Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Scania Tawi la Tanzania, Bw. Ali Dar.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwa katika picha na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, walipokutana na kufanya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden, ikiwa na ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden mwezi Septemba, 2023.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias (wanne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Sweden na Tanzania baada ya kumalizika kwa mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma, ambapo wamejadili masuala mtambuka ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden, ikiwa na ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden mwezi Septemba, 2023. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha)

Na Benny Mwaipaja, Dodoma

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, , ambaye ameahidi kuwa nchi yake, kupitia Taasisi zake likiwemo Shirika la Dhamana la nchi hiyo (EKN), itashiriki kugharamia ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.

Katika mazungumzo yao Mhe. Nchemba ameishukuru Sweden kwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania, ikiwemo kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Lot 2, kipande kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 96 na kwa utayari wa nchi hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kujenga reli kipande cha tatu na cha nne.

” Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameelekeza mradi wa reli ya kisasa SGR, uanze kufanyakazi kuanzia mwezi Juni mwaka 2024, na tunaishukuru Sweden kwa kufanikisha ujenzi wa mradi huo kipande cha pili cha kuanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Dingida na tunasubiri ufadhili wa kipande cha tatu na cha nne baada ya kukamilisha masharti ya kufanya upembuzi kuhusu mazingira na jamii suala ambalo liko katika hatua za mwisho kutekelezwa” alisema Mhe. Dkt. Nchemba

Wakizungumza katika mkutano huo, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliyeambatana na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm, wamesifu uhusiano imara uliopo kati ya nchi hizo mbili na kuahidi kukuza zaidi uhusiano wa kiuchumi kwa faida ya pande hizo mbili.

Mhe. Balozi Macias alisema kuwa nchi yake inasubiri kukamilika kwa masuala yaliyokubaliwa ikiwemo masuala ya mazingira na jamii ambao utekelezaji wake unatarajia kukamilika hivi karibuni.

Ziara ya Balozi huyo wa Sweden Mhe. Charlotta Ozaki Macias, na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Mhe. Cecilia Ekholmni ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba, aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden, na kukutana na uongozi wa Shirika la Dhamana la nchi hiyo (EKN), ambalo limetoa usaidizi katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) upande wa malighafi ya ujenzi, vitendea kazi, mifumo ya umeme, mitambo na teknolojia.

Previous articleWANANCHI 9,717 NJOMBE KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI IGONGWI
Next articleRAIS SAMIA ATETA NA RAIS WA TAASISI YA BIG WIN PHILANTHROPY IKULU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here