Featured Kitaifa

RUFAA YA MARIA NGODA ALIYEFUNGWA MIAKA 22 KWA KUKUTWA NA NYAMA YA SWALA YASIKILIZWA .

Written by mzalendo

HAKAMA Kuu ya Mkoa wa Iringa chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta leo Februari 1, 2024 imesikiliza kesi ya Rufaa  Namba 84101/2023 kati ya Maria Ngoda dhidi ya Jamuhuri.

Akiongoza jopo la Mawakili upande wa mkata rufaa Wakili Moses Ambwindile amesema leo wametetea sababu zao za  Rufaa 14 mbele ya Jaji Mfawidhi.

Aidha Jaji Mgetta ameahirisha shauri hilo mpaka hapo kesho tarehe 2 Februari 2024. 

Mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) alihukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3,2023.

About the author

mzalendo