Featured Kimataifa

MAJALIWA ASHIRIKI MKUTANO WA TATU WA KUSINI WA KUNDI LA 77 NA CHINA

Written by mzalendo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye umoja wa Mataifa Balozi Hussein Kattanga, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Tatu wa Kusini wa Kundi la 77 na China kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Rwenzori uliyopo katika Hoteli ya Speke Resort, Kampala Uganda Januari 21, 2024.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa akimkabidhi rasmi Rais wa Uganda Yoweri Museveni uenyekiti wa Kusini wa Kundi la 77 na China, Kampala nchini Uganda, Januari 21, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Nchi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Shakhboot Bin Nahyan, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Tatu wa Kusini wa Kundi la 77 na China kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Rwenzori uliyopo katika Hoteli ya Speke Resort, Kampala Uganda Januari 21, 2024.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishiriki Mkutano wa Tatu wa Kusini wa Kundi la 77 na China kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Rwenzori uliyopo katika Hoteli ya Speke Resort, Kampala Uganda Januari 21, 2024. Mheshimiwa Majaliwa amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendo