Featured Kitaifa

KATIBU MKUU UCHUKUZI ATEMBELEA BANDA LA MSCL ZANZIBAR.

Written by mzalendo
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara (wa kwanza kulia) akizungumza na watumishi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) walipotembelea banda hilo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar. Wa kwanza kushoto ni Afisa Uhusiano kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Abdulrahman Salim Ally na wa pili kushoto ni Afisa Masoko kutoka Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Victoria John Mwakalasya
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara akisaini kitabu kwenye banda la Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) alipotembelea banda hilo akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Ali Possi kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
………….
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi  Prof Godius Kahyarara leo amepata fursa ya kutembelea banda la Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) lilipo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Zanzibar. KM ameipongeza MSCL kwa kushiriki katika Maonesho hayo kwani ni fursa nzuri ya kuwasiliana, kujifunza na kubadilishana taarifa na maarifa na wadau wa sekta ya usafirishaji.
Pamoja naye, viongozi wengine waliopata fursa ya kufika banda la MSCL ni pamoja na NKM Uchukuzi Dkt. Ally Possi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC Nahodha Musa H Mandia na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Ndg Mohamed M Salum.
na banda letu lipo sanjari na mabanda ya taasisi nyingine za Wizara ya Uchukuzi.
Leo Tumetembelewa na Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa Bodi TASAC na DG wa TASACA

About the author

mzalendo