Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara Ndg. Abdulrahman Kinana  Akimzungumzia  Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi Katika Kikao  Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Balozi mstaafu Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa Katika Kikao  Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, Akifurahi Pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara Ndg. Abdulrahman Kinana na  Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Emmanuel Nchimbi   leo 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

……..

Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa imefanya kikao Maalum tarehe 15 Januari, 2024, Zanzibar, chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kikao hicho kilitanguliwa na Semina kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kuanzia tarehe 13 – 14 Januari, 2024. Katika Semina hiyo wajumbe walipewa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wake ikiwemo: –

1. Mradi wa Bwawa la Umeme wa Julius Nyerere (JHPP) na mipango ya kuboresha hali ya umeme Nchini.

2. Mradi wa Reli ya “Standard Gauge Railway (SGR)”.

3. Ujenzi wa daraja la John Pombe Magufuli (Kigongo – Busisi).

4. Utekelezaji wa Ilani ya CCM, kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

5. Hali ya Mashirika ya Umma Nchini na Mageuzi yanayohitajika.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilipokea taarifa mbalimbali ikiwemo: –

1. Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji mwaka 2024.

2. Maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 47 ya Kuzaliwa kwa CCM.

Aidha, kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimepokea pendekezo la Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kuhusu jina la Katibu Mkuu wa CCM. Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa wameridhia kwa kauli moja pendekezo hilo na kumchagua Ndugu Balozi (Mst) Dkt. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

 

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kimeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Ndugu Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 kwa upande wa Zanzibar na kufanikisha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Vile vile, kikao hicho kimepongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kutekeleza kwa ufanisi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025.

 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Previous articleMNYETI: “MAAFISA MIFUGO NENDENI KWA WAFUGAJI, ACHENI KUWA WAKUSANYA MAPATO.”
Next articleSERIKALI INATAMBUA KAZI KUBWA INAYOFANYWA NA WANACHAMA WA TALGWU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here