Featured Kitaifa

SERIKALI INATAMBUA KAZI KUBWA INAYOFANYWA NA WANACHAMA WA TALGWU

Written by mzalendo

NAIBU WaziriOfisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua  Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,amesema Serikali  inatambua kazi kubwa inayofanywa na Wanachama wa TALGWU katika maeneo yao ya kazi katika kusimamia utekelezaji wa maendeleo ya nchini.

Mhe.Katambi ameyasema hayo leo Januari 15,2024 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU). 

Katambi ,amesema Serikali itaendelea kulinda na kuendeleza haki za wafanyakazi nchini huku ikitambua, kuheshimu na kuuenzi mchango wa Watumishi wa Umma ambao ni Wanachama TALGWU.

“Waajiri kuhakikisha  wanafuata matakwa ya sheria za kazi za nchi na  kudumisha mahusiano mema kazini kwa manufaa yenu wenyewe na wafanyakazi wenu na  Utashi wa Serikali katika kutekeleza wajibu wake wa kulinda haki za wafanyakazi nchini umejidhihirisha wazi kupitia hatua za kisheria na za kiuchumi ambazo imekuwa inatekeleza,” 

Na kuongeza kuwa”Tunatambua kuwa wengi wenu mnafanya kazi katika mazingira magumu lakini  Serikali haitachoka kuzifanyia kazi kero na changamoto zenu na kutafuta njia mbalimbali za kuzipatia ufumbuzi sambamba na kuendelea kuboresha mazingira ya kazi,”amesema Katambi

Kuhusu Changamoto Mhe.Katambi,amewahakikishia TALGWU kuwa Serikali ipo tayari kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha wafanyakazi wanatekeleza majukumu yao kwa amani huku changamoto walizonazo zikiwa zinapatiwa ufumbuzi na Serikali chini ya uongozi madhubuti wa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Aidha amewataka wanachama wote wa TALGWU kutambua kuwa ulinzi wa haki za wafanyakazi huanzia kwa wao wenyewe kwa kuzingatia dhana ya haki ba wajibu hivyo chana hicho kinapasawa kuwakumbusha wafanyakazi kujiepusha na vitendo vinavyoendekea kinyume na misingi na maadili ya utumishi wa umma.

 “Wafanyakazi kama hawatajiepusha na matendo hayo maovu basi watafanya kazi ya kutetea na kulinda haki zao kuwa ngumu kwao na wadau wengine kama sisi. Lazima wakati wote tukumbuke kuwa kudai haki kunaenda sambamba na kutimiza wajibu,”amesisitiza Katambi

Kwa upande wake  Mwenyekiti  wa TALGWU Taifa Bw.Tumaini  Nyamhokya amesema kuwa kuna kilio Kikubwa cha wafanyakazi walio na elimu ya darasa la Saba ambao mishahara yao kati ya miezi mitatu hadi sita haikulipwa ,zile siyo fedha za hisani ni mishahara yao lakini pia na hata walivyosimama walisimama kimakosa kwani  hata barua zao tunazo.

Awali Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Bw.Rashid  Mtima,ameiomba serikali kutatua changamoto na kero  zinazowakabili ikiwemo changamoto ya kulipa  Leseni ya kutoa huduma kwa watumishi  wa kada ya Afya.
Bw.Mtima amesema kuwa kuna manung’uniko na malalamiko makubwa kwa watumishi wa kada ya Afya yani Wauguzi, Wafamasia, Wataalamu wa Maabara, Wataalamu wa Mionzi na Wafiziothelapia kutakiwa kujilipia ada ya Leseni  ya kila Mwaka huku wa kuwa wanatekeleza majukumu ya kutoa huduma kwa umma.
“Iwapo watashindwa kulipa ada hiyo wanakosa haki  ya kupandishwa madaraja  na kushindwa kubadilishwa  vyeo, ikumbukwe kuwa watumishi hawa hawafanyi biashara kwa leseni hizo isipokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku kwa maendeleo ya Taifa letu” amesema  Bw.Mtima

NAIBU WaziriOfisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akizungumza wakati akifungua  Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

NAIBU WaziriOfisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi,akisisitiza jambo wakati akifungua  Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa TALGWU Taifa Bw.Tumaini Nyamhokya,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Ndg. Rashid  Mtima,akitoa taarifa ya Kikao cha Baraza Kuu TALGWU Taifa kilichofanyika leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

BAADHI ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Naibu  WaziriOfisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,Mhe.Patrobas Katambi (hayupo pichani), wakati akifungua  Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) leo Januari 15,2024 jijini Dodoma.

About the author

mzalendo