Mkurugenzi wa Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA), Usekelege Mpulla, amewataka watumishi wa tume kufanya kazi kwa uzalendo,weledi,uadilifu,na ufanisi pamoja na kuzingatia haki katika kuwahudumia wananchi, ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa waajiri na waajiriwa katika kutatua migogoro ya kikazi kwa mwaka 2024.

Wito huo umetolewa leo 29 Disemba,2023 katika ofisi za Makao makuu ya tume Mkoani Dodoma, wakati akitoa salamu za mwaka mpya wa 2024 kwa wadau,wafanyakazi, na wananchi wote, ikiwa ni Pamoja na kuelezea mikakati ya mwaka unaofuata katika kuhakikisha tume inatekeleza majukumu yake na kuongeza utendaji kazi katika kushughulikia migogoro ya kikazi Tanzania Bara.

Mpulla ameongeza kwamba, tume imejipanga vyema kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wadau mbalimbali wenye migogoro ya kikazi, na kwakutambua umuhimu wa kuboresha shughuli za tume wameamua kuanza na kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa tume ili kuweza kubaini mapungufu na kuboresha utendaji kazi.

“Tumejipanga kwaajili ya mwaka 2024, tutamaliza na kikao cha tathmini ili kujijua tumekosea wapi tuje na mikakati mikubwa ya kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yetu wenye kuleta tija kwa Tanzania lakini kuweza kumnufaisha kila mdau anaenufaika na huduma za tume”amesema.

Aidha, Mpulla amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa Pamoja na kuisaidia tume kuweza kutekeleza majukumu yake.

Vilevile, amemshukuru Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof. Joyce ndalichako,pamoja na katibu mkuu kwa mchango mkubwa wanaotoa kuhakikisha tume inahudumia wananchi na kuendesha shughuli mbalimbali za tume.

Hata hivyo, tume ya usuluhishi na uamuzi inayohusika na kusuluhisha Pamoja na kuamua migogoro ya kikazi Tanzania bara, inatarajia kuwa na kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa tume ili kuboresha huduma na uwajibikaji ndani ya taasisi hiyo, kinachotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 04 hadi 06, Januari,2024.

Previous articleDKT. BITEKO AWASILI MKOANI SHINYANGA
Next articleSERIKALI KUJENGA KITUO KIPYA CHA AFYA GENDABI, HANANG

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here