OR-TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI nayeshughulikia Afya, Mhe. Dkt. Festo Dugange amemwelekeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ifikapo Januari 3,2024 ujenzi wa shule ya Sekondari ya kata ya Kitwiru inayogharimu sh.milioni 583 uwe umekamilika.
Akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa shule hiyo, Dkt. Dugange ameusisitiza uongozi wa manispaa hiyo kuongeza kasi ya usimamizi na shughuli zifanyike usiku na mchana ili ifikapo Januari 08,2024 wanafunzi waingie madarasani.
“Hakikisheni inapofika januari 03,2024 muwe mmekamilisha majengo yote ya msingi tutenge muda sasa wa usiku na mchana maana tuna wiki mbili tu watoto lazima waanze kidato cha kwanza hapa,”amesema.
Kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kutawapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umba wa zaidi ya kilomita 13 kufuata masomo katika shule ya Sekondari Ipogolo.