Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi amewataka madereva wa Malori yatokayo ndani na nje ya Nchi yanayobeba makaa ya mawe Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili waweze kuepuka ajali zisizo za lazima kwao na kwa watumiaji wengine wa barabara.

Ameyasema hayo Desemba 22, 2023 katika kijiji cha Amani Makolo Barabara ya Kitai – Ruanda katika Maeneo ya machimbo ya makaa ya mawe yalipo Halmashauri ya Mbinga Vijijini Mkoani Ruvuma.

Pia SACP Ng’anzi alieleza kuwa Jeshi la Polisi halitakuwa na muhali kwa yeyote atakaebainika kuvunja sheria kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwa pamoja na kukamatwa, kufunguliwa mashtaka, kufungiwa leseni na kufikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Aidha aliwataka Madereva hao kuhakikisha wanajiendeleza kimasomo katika vyuo mbalimbali ili waweze kukuza fani zao na kupata vyeti ambavyo vitawatambulisha sifa zao na kuhakikisha wanapata leseni pamoja na kuhakiki leseni zao za udereva kabla ya ukomo wa sheria kuwafikia.

Sambamba na hilo alimtaka Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoan wa Ruvuma Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Issa Milanzi kuhakikisha Kikosi kinaimarisha doria za Usalama Barabarani na Ukaguzi wa vyombo moto ili kuweza kuwabaini wale wachache wanaotenda kinyume cha sheria na kuwachukulia hatua.

SACP Ng’anzi alimalizia kwa kukagua namna mifumo ya Jeshi la Polisi ya Usalama Barabarani kama Road accident management information (RAMIS), Traffic Management System (TMS) na Mfumo wa utoaji Leseni (OGD) ambayo imeanza kutumiwa na vikosi vya Usalama Barabarani Tanzania bara na visiwani.

Previous articleDKT.DUGANGE ATOA WIKI MBILI UJENZI WA SHULE KITWIRU UKAMILIKE
Next articleWAZIRI JAFO AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here