Featured Kitaifa

WIZARA YA AFYA ,WADAU WA AFYA MOJA WAJADILI KUKABILI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Written by mzalendoeditor

 

Na.Elimu ya Afya kwa Umma.

Tanzania inajivunia kuanzishwa kwa Kurugenzi Maalum ya Uratibu wa Afya Moja ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yenye lengo la kuoanisha afua katika Wizara zote ili kudhibiti Magonjwa yanayohitaji ushirikishwaji wa Sekta mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Kikao Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Tumaini Haonga katika kikao cha uchambuzi wa awali wa mbinu ya Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele

Dkt. Haonga amesema Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani imefanya kikao cha wadau wa Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kuanzia tarehe 13 Disemba Hadi tarehe 15 Disemba 2023 Mjini Morogoro.

Kikao kimekutanisha Wadau kutoka Wizara ya Afya na Wizara mtambuka (OR TAMISEMI, OMR-Mazingira, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maji, Kilimo, Mifugo, Elimu) Taasisi za Utafiti, Vyuo Vikuu, na Wadau wa Maendeleo

Aidha, Kikao hicho kililenga kufanya uchambuzi wa awali (situation analysis) wa mbinu ya Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hasa yale yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Zaidi ya hayo, Dkt. Haonga amesema Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDCP), ulianzishwa mwaka 2009 chini ya Wizara ya Afya ili kuweza kuratibu Magonjwa haya.

“Licha ya juhudi hizi zilizoratibiwa, bado Magonjwa ya NTDs hasa yanayoambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu yanaendelea kupokea uangalizi duni kutoka kwa mifumo ya huduma za afya, taasisi za utafiti, Elimu na watunga Sera”. Amesema Dkt. Haonga.

About the author

mzalendoeditor