Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa elimu kuhusu Uanzishwaji wa Klabu za Kidijiti kwa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania zenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi (vijana) kuwa wabunifu na wavumbuzi kwa kutumia Digitali ili kuongeza na kukuza matumizi ya TEHAMA.
TCRA imetoa elimu hiyo leo Jumamosi Desemba 16,2023 wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tanzania Heads of Secondary Schoool Association – TAHOSSA) uliofanyika Jijini Mwanza.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo amesema TCRA itaendelea kuhamasisha ubunifu na uvumbuzi katika klabu za kidijiti zilizoanzishwa na zitakazoanzishwa ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo waratibu wa klabu za kidijiti ili waweze kuzisimamia vyema ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.
“Uanzishwaji wa Klabu hizi za Kidijiti siyo wa holela ni lazima kuwe na usimamizi maalumu ili kulinda maadili ya Mtanzania. Pia TCRA itaandaa mashindano ya klabu za kidijiti, na klabu zitakazofanya vizuri kwa vigezo vitakavyowekwa zitazawadiwa”,amesema Mhandisi Mihayo.
“TCRA inaamini Wakuu wa Shule mtasaidia uanzishwaji wa klabu za kidijiti katika shule zenu. Ikumbukwe kuwa klabu hizi hazina tofauti na klabu nyingine za masomo kama Hisabati, Kiingereza n.k. Tunapoelekea kwenye uchumi wa kidijiti, matumizi ya TEHAMA hayaepukiki hivyo ni tunapaswa tuwaandae vijana wetu”,amesema Mhandisi Mihayo.
Mhandisi Mihayo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha walimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao pia kujiepusha na matapeli ambao wanatumia vibaya mitandao.
Amesema endapo wakipata ujumbe wa utapeli watume ujumbe huo kwenda namba 15040.
“Matumizi ya Digitali hayaepukiki. Tumieni mitandao ya kijamii kujiletea maendeleo, hii mitandao inaweza kukuharibia au kukujenga. Wafundisheni pia wanafunzi wenu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao endapo utaona ujumbe wa kitapeli au udhalilishaji toa taarifa. Lakini pia mkumbuke kuwa taarifa yoyote unayoiweka mtandaoni huwa haipotei. Mnachapisha vitu vingi mtandaoni kumbukeni kuwa mtandao hausahau kila kinachowekwa”,amesema Mhandisi Mihayo.
“Magroup ya Whatsapp hayasajiliwi lakini Admin wanabeba dhamana wa mambo yote yanayoendelea kwenye group, wao ndiyo viranja wa makundi sogozi Walimu tusaidieni kuwaambia vijana kuwa wanapotumia vibaya mitandao ya kijamii wanaweka rehani maisha yao”,ameongeza Mhandisi Mihayo.
Meneja huyo wa TCRA Kanda ya Ziwa pia amewakumbusha watumiaji wa simu kuweka nywila (Password) ngumu kwenye simu zao ili kulinda taarifa zao na kuwa salama.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
“Ili kulinda taarifa zako weka Nywila ngumu kwa sababu simu yako haina ubia na mtu mwingine ndiyo maana tunasajili kwa kutumia vidole, usimpe simu yako mtu yeyote”,amesema
“Pia unapotaka kusafirisha kipeto au kifurushi hakikisha mtoa huduma amesajiliwa kwa kupiga *152*00# kisha bonyeza namba 3 halafu namba 9 ili kuepuka kusafirishiwa kifurushi au kipeto kwa kutumia kampuni ambayo haina leseni ya usafirishaji”,amesisitiza.
Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa TEHAMA TCRA, Irene Kahwili amesema TCRA inaendelea kusimamia Sekta ya Mawasiliano ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali nchini na katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ili kuhakikisha Sekta ya Mawasiliano inatoa mchango katika maendeleo ya nchi na kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi wa kidijiti.
Amefafanua kuwa Mwaka 2022, TCRA ilikuja na wazo la kuanzisha klabu za kidijiti kwa lengo la kupanda mbegu ya TEHAMA tangu awali na kuibua ubunifu na uvumbuzi na vipaji kwa watoto na vijana.
Amesema Klabu za Kidijiti ni Jukwaa linalowakusanya wanafunzi wanaopenda masomo ya teknolojia ili kuongeza weledi wa kidijiti,
majadiliano na kufanya shughuli mbalimbali kwa kutumia teknolojia na vifaa vya kidijiti lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanafunzi kushiriki katika utamaduni mpya wa kidijiti.
Ameongeza kuwa walengwa ni Wanafunzi wa ngazi zote za kitaaluma (Chekechea hadi Chuo kikuu), ikiwa ni pamoja na wale wa taaluma za ufundi na zisizo za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Amezitaja Tunu za Klabu ya Kidijiti kuwa ni Uwezeshaji (Kuwatia moyo na kuwapa wanachama fursa ya kupata ujuzi), Ubunifu (Kuhimiza udadisi, ubunifu na mawazo mapya ya wanachama),
Kujenga Timu (Kukuza maadili ya uwazi, uaminifu, heshima na ushirikiano miongoni mwa wanachama) pamoja na Weledi (Kuzingatia viwango vya juu vya taaluma katika shughuli za klabu na mawasiliano).
Amesema kujiunga na Klabu ya Kidijiti ni bure na hiari na Wanafunzi wote wanastahiki kujiunga na Klabu ya Kidijiti ndani ya Taasisi zao ambapo uongozi wa taasisi utawasaidia wanachama watarajiwa wa klabu kuanzisha klabu ya kidijiti kisha wataisajili klabu kwenye mfumo wa Klabu za Kidijiti https://digitalclubs.tz
Kwa upande wake, Afisa Masoko TCRA Kanda ya Ziwa, Benadetha Clement amesema TCRA ilianzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania namba 12 ya mwaka 2003 baada ya kuunganishwa kwa zilizokuwa Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC) na Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) ambapo utekelezaji wa majukumu ya TCRA unaofanywa kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayosimamia Sekta ya Mawasiliano.
Ameongeza kuwa TCRA inasimamia mawasiliano ya Simu na Intaneti, Utangazaji pamoja na Posta.
“Majukumu ya TCRA ni pamoja na kutoa leseni na kusimamia makampuni yanayotoa huduma za simu, utangazaji, Intaneti, Posta na Usafirishaji wa Vifurushi na Vipeto”,amesema.
Naye Rais wa TAHOSSA, Dennis Otieno ameishukuru TCRA kuwapatia elimu ya uanzishwaji wa Klabu za Kidijiti sambamba na elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii yakiwemo Makundi ya Whatsapp na Facebook.
“Elimu tuliyopewa ni nzuri na inatujenga kutokana na kwamba tunatumia teknolojia kila siku. TCRA wasichoke, waendelee kutoa elimu kwenye shule zetu”,amesema.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza leo Jumamosi Desemba 16,2023 wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tanzania Heads of Secondary Schoool Association – TAHOSSA) uliofanyika Jijini Mwanza.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA). Kushoto ni Meneja wa Sehemu ya Masuala ya Wateja na Watumiaji TCRA Thadayo Ringo
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Afisa Masoko TCRA Kanda ya Ziwa, Benadetha Clement akitoa mada kuhusu TCRA wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Afisa Masoko TCRA Kanda ya Ziwa, Benadetha Clement akitoa mada kuhusu TCRA wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Afisa Mkuu wa TEHAMA TCRA, Irene Kahwili
akitoa mada kuhusu Klabu za Kidijiti wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)

Rais wa TAHOSSA, Dennis Otieno akizungumza na waandishi wa habari
Maafisa kutoka TCRA wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)
Meneja wa Sehemu ya Masuala ya Wateja na Watumiaji TCRA Thadayo Ringo ( wa pili kushoto) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 18 wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA)