Featured Kitaifa

WANANCHI WILAYANI NYASA WAHIMIZWA KUFANYA SHUGHULI ZISIZOHARIBU MAZINGIRA ZIWA NYASA

Written by mzalendo

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa. 

Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akizungumza wakati wa ziara ya kikazi Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa

Watumishi na viongozi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

…….

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewahimiza wananchi kufanya shughuli zisizoharibu mazingira ya Ziwa Nyasa.

Ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Hifadhi ya Ardhi ya Bonde la Ziwa Nyasa.

Mhe. Khamis amesema kuwa ni muhimu shughuli za kilimo ziifanyike lakini zizingatie kuboresha na si kinachosabisha uhaharibifu wa mazingira yanazunguka bonde hilo.

Aidha, amewataka wataalamu hao kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi ikiwemo upandaji wa miti kwa mujibu wa maelekezo ya Serikal ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri Khamis Sanjari na hilo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Nyasa kwa kusimamia vyema Mradi wa Kuhifadhi Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa.

Miongoni mwa shughuli zinazofanyika kupitia mradi huo ni utengenezaji wa majiko banifu ambayo hupunguza matumizi ya kuni na mkaa hivyo kasi ya ukataji miti hupungua au kuisha kabisa.

Kutokana na hatua hiyo, Naibu Waziri Khamis amewahimiza wataalamu wa mazingira kutoa elimu ya matumizi ya majiko hayo na kupanua wigo wa utengenezaji ili kuongeza ufanisi wa mradi.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni mbili una ambazo zinasaidia kuiwezesha jamii kufanya shughuli mbadala ili kukabiliana na changamoto za kimazingira na unatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Ludewa (Njombe), Mbinga na Nyasa (Ruvuma).

About the author

mzalendo