Featured Michezo

RAIS DKT.MWINYI AWEKA JIWE LA MSINGI VIWANJA VYA NJE YA UWANJA WA AMAAN STADIUM ZANZIBAR

Written by mzalendo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi wa ujenzi wa Viwanja vya nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar  (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN inayojenga Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar. Bw. Ilhan Karadeniz, hafla hiyo.

Khadija Khamis- Maelezo 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema  Serikali ya Zanzbar itaendelea kuweka mazingira bora ya michezo ili kuimarisha vipaji vya wanamichezo.

Dkt. Mwinyi ametoa kauli hiyo katika hafla  ya  uwekaji  wa  jiwe la msingi, viwanja vya nje ya  Uwanja wa Amani Studium pamoja na ujenzi mpya wa Miundombinu ya Uwanja huo. 

Amesema azma ya Serikali ni kuimarisha sekta ya michezo  kwa kuendeleza na kuibua vipaji vya wanamichezo ili  kuleta maendeleo  Nchini.

 “Sasa hivi hatuna shaka vipaji tunavyo vya michezo mbalimbali tunachohitaji mazingira bora,”alisema Dkt. Mwinyi.

Aidha alieleza kuwa uwanja huo utatumika kwa michezo ya aina mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu, judo, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mkono, na mengineyo.

Dkt. Mwinyi ameipongeza kampuni ya Orkun ya  Uturuki kwa juhudi waliyoifanya ya kukamilisha ujenzi  huo kwa wakati na kwa kiwango cha kimataifa.

Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Mwinyi Kwa jitihada zake kubwa katika kusimamia Michezo Nchini.

Aidha, Waziri Tabia amesema Uwanja huo unakila sifa  na vigezo vya kuitwa Amani Sports Complex hivyo amemuomba Rais wa Zanzibar kulitumia jina hilo badala ya Amani Studium.

Uwanja wa Amaan Stadium unatarajiwa kuzinduliwa Rasmin hivi karibuni katika Shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutumika katika michuano ya kombe la Mapinduzi Cup.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Viongozi mbalimbali, alipowasili katika Uwanja wa Amaan  kwa ajili ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi  wa viwanja vya nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar, hafla hiyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuweka Jiwe la Msingi wa ujenzi wa Viwanja vya nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar  (kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN inayojenga Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar. Bw. Ilhan Karadeniz, hafla hiyo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN inayojenga uwanja huo Bw. Ilhan Karadeniz, wakati akitembelea Viwanja vya Nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo, hafla hiyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN inayojenga uwanja huo Bw. Ilhan Karadeniz, wakati akitembelea Viwanja vya Nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo, hafla hiyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN inayojenga uwanja huo Bw. Ilhan Karadeniz, wakati akitembelea kiwanja cha ndani cha michezo wa mpira wa Kikapu katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi huo, hafla hiyo

BAADHI ya Wafanyakazi wa Kampuni ya ORKUN inayojenga Uwanja wa Amaan Zanzibar na Wananchi wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanja vya Nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar, hafla hiyo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia na kuwapongeza  Wanafunzi wa Skuli ya Jangombe Unguja Fadhila Ibrahim na Sharifa Somea, baada ya kumaliza kutowa burudani ya Ngoma ya Kunguwia, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanja vya Nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar.

WATOTO wa Kikundi cha Mchezo wa Karate cha Island Warriors  Zanzibar wakionesha umahiri wa mchezo huo wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanja vya Nje ya Uwanja wa Amaan Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika jana usiku 14-12-2023.(Picha na Ikulu)

About the author

mzalendo