Featured Kitaifa

TANESCO ZINGATIENI MASLAHI YA WATUMISHI WENU ILI KUONGEZA UFANISI NA UBUNIFU-MHE.KATAMBI

Written by mzalendo

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Patrobas Katambi, akizungumza wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la 53 la wafanyakazi wa shirika hilo linalofanyika kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji jijini Dodoma.

Na Paul Mabeja, DODOMA

 

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Patrobas Katambi, amelitaka Shirika la umeme nchini (TANESCO) kuzingatia maslahi ya watumishi wake ili kuongeza ufanisi na ubunifu katika kutekeleza majukumu yao.

Katambi, alibainisha hayo leo Desemba 12,2023 jijini Dodoma , alipokuwa akifungua mkutano wa baraza kuu la 53 la wafanyakazi wa shirika hilo linalofanyika kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji.

Alisema ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa watumishi ndani ya shirika hilo maslahi ya watumishi yanapaswa kupewa kipaumbele ili kuongeza uwajibikaji.

“Ili kuongeza ufanisi wa shirika letu hili ambalo tunalitegemea katika uzalishaji wa umeme mnapaswa kuzingatia maslahi ya watumishi wenu kwa kuwapa motisha, posho, kupandishwa vyeo ili kuwaondolea stres watumishi na kuongeza tija an ubunifu katika shirika hili tunalolitegemea kwa kuzalisha nishati ya umeme nchini”alisema Katambi

Aidha, Katambi aliwataka watumishi wa shirika hilo kuzingati wajibu wao katika utekelezaji wa majukumu kabla ya kudai haki zao.

“Kabla ya kudai haki zetu lazima tuangalie wajibu wetu katika maeneo yetu tumeutimiza kwa ukamilifu suala la umeme nchini ni jambo la muhimu sana hivyo tunapaswa kutimiza majukumu yetu ili kuondoa malalamiko ya mgao wa umeme nchini”alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Gissima Nyamo-hanga alisema mkutano wa baraza hilo utafanyika kwa siku mbili ukiwa lengo la kujadilia mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya kiutendaji.

Kadhalika, alisema maagizo yote yalitolewa na Naibu waziri Katambi watayafanyia kazi ili kuongeza ufasi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa watumishi wao.

“Baraza kuu la wafanyakazi ni chombo ambacho pia majukumu yake ni kuangalia maslahi na haki za wafanyakzi hivyo pia katika kikao chetu tutakwenda kujadili masuala ya maslahi kwa watumishi na haki zao”alisema

Hata hivyo, akizungumzi kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme nchini alisema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeongeza uzalishaji katika vyanzo vilivyopo nchini ikiwemo Mtera,Kihanzi na Kidatu.

 

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Patrobas Katambi, akizungumza wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la 53 la wafanyakazi wa shirika hilo linalofanyika kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji jijini Dodoma.

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Patrobas Katambi,akisisitiza jambo  wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la 53 la wafanyakazi wa shirika hilo linalofanyika kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu  Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu Patrobas Katambi, (hayupo pichani)  wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la 53 la wafanyakazi wa shirika hilo linalofanyika kwa siku mbili kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji jijini Dodoma.

About the author

mzalendo