Featured Kitaifa

KAMPUNI YA BIMA YA PHOENIX TANZANIA YABADILISHA JINA KWENDA MUA TANZANIA KUAKISI UBORA NA UKUAJI WA HUDUMA

Written by mzalendoeditor

 

Kampuni ya Phoenix Assurance Tanzania, mtoa huduma mkuu wa bima, imetangaza kubadili jina kwenda MUA Tanzania hatua inayoashairia dhamira yake endelevu ya kuwahudumia watanzania.

Hatua ya kubadili chapa inaendana na mkakati wa kikanda ambao umejikita katika uboreshaji huduma wa mara kwa mara. Ujio wa MUA Tanzania unatoa mwelekeo mpya katika utoaji wa huduma zinazongatia ubora, viwango, ubunifu na weledi kwa watanzania.

Pia, kampuni hiyo imejikita katika utoaji wa huduma za kidigitali ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja wake.

Zoezi la ubadilishaji wa chapa limezingatia matakwa na mahitaji ya wadau wote muhimu. Kampuni ya Phoenix Assurance imefanya kazi kwa ukaribu zaidi na Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa na kukidhi matakwa ya kisheria. “Tunatarajia kufanya kazi kwa ukaribu na mamlaka zote za usimamizi na wadau wetu muhimu ili kuendelea kuijenga sekta ya bima nchini Tanzania kwa kutoa huduma bora na kuleta suluhu zinazokidhi mahitaji ya watu,” alisema Jérôme Katz, Mkurugenzi Mkuu wa MUA Tanzania.


Nembo mpya ya MUA Tanzania inaashiria dhamira ya kampuni katika ukuaji, uimara, na uthabiti na mtazamo wa mbele. Chapa mpya inabeba imani na uthabiti ambao kampuni imejenga kwa zaidi ya miaka 25 nchini Tanzania na zaidi ya miaka 110 katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Wakati jina likibadilika, MUA Tanzania inawahakikisha wateja na washirika wake kuwa misingi na malengo ya biashara yanabaki vile vile na thabiti zaidi. Kampuni imejizatiti katika kuhakikisha inatoa huduma bora za bima ambazo zitakidhi mahitaji ya watu binafsi na biashara hapa Tanzania.

“Dhamira yetu katika ubora, uadilifu, na kukidhi kiu ya wateja wetu haitabadilika” alisema Jérôme Katz “Kwa kubadilika kuwa MUA Tanzania hatubadili jina pekee, tunaonesha nia na utayari wetu kwa wateja na washirika wetu katika kutoa huduma na suluhu za bima zenye ubora zaidi,” alisema.

MUA Tanzania inaendelea na nia yake ya dhati ya kuchangia maendeleo chanya ya uchumi na jamii ambayo imekuwa ikiihudumia toka mwaka 1999. Kampuni inaendelea na nia ya dhati ya kuwajibika kwa jamii na juhudi zinazonufaisha watu na jamii kwa ujumla.
Katika mwanzo wa safari hii mpya, MUA Tanzania, kampuni inatoa shukurani zake kwa wateja wote, washirika, na wadau kwa kuendelea kuwaamini na kuwaunga mkono.

Kuhusu MUA Tanzania

MUA Tanzania ni mtoa huduma bora wa bima aliyejitolea kutoa suluhisho za kibunifu na za uhakika za bima kwa watu binafsi na wafanyabiashara nchini Tanzania. Ikiwa na historia kubwa ya uaminifu na uadilifu, MUA Tanzania imejizatiti kutumikia jamii na kuchangia maendeleo ya taifa.

Kwa taarifa zaidi tembelea www.mua.co.tz

MUA Stakeholders From left
1. Mr. Vikas Varma
2. Mr. Amal Somaiya
3. Miss Sonia Somaiya
4. Mr. Joerg Weber
5. Mr. Samuel Mwiru
6. Mr. Jerome Katz
7. Mr. Isaac Kiwango
8. Dr. Wilbert Kapinga
9. Mr. Ashraf Mushi

About the author

mzalendoeditor