Featured Kitaifa

DKT.DUGANGE ATEMBELEA KAMBI YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG’

Written by mzalendoeditor

Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange akiwa ameambatana na Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga wametembelea shule ya Msingi Gendabi eneo ambalo ilipo kambi ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Hanang mkoa wa Manyara.

Katika kambi hiyo wameshuhudia zoezi la ugawaji wa misaada inayoendelea kutolewa huku wengine wakichukuliwa na ndugu na jamaa wakati serikali ikiendelea na taratibu za kusaidia waathirika hao.

About the author

mzalendoeditor