Featured Kitaifa

UWT YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WAKE

Written by mzalendo

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Bi. Marry Chatanda,akizungumza  wakati   akifungua mafunzo ya makatibu wa UWT mikoa, wilaya na viongozi wa umoja huo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao leo Desemba 11,2023 jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Bi. Marry Chatanda,akizungumza  wakati   akifungua mafunzo ya makatibu wa UWT mikoa, wilaya na viongozi wa umoja huo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao leo Desemba 11,2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jokate Mwegelo,akielezea lengo la  mafunzo ya makatibu wa UWT mikoa, wilaya na viongozi wa umoja huo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao leo Desemba 11,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Bi. Marry Chatanda, ametoa rai kwa watendaji na viongozi wa umoja huo kuzingatia mafunzo wanayoyapata kwa lengo la kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Chatanda ametoa wito  huo leo Desemba 11,2023 jijini Dodoma wakati leo  akifungua mafunzo ya makatibu wa UWT mikoa, wilaya na viongozi wa umoja huo yenye lengo la kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mafunzo haya yatawajengea uelewa viongozi na watendaji wa UWT katika kutekeleza majukumu yao kwa kuongeza wanachama, kutambua wapiga kura wapya na kusimamia utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM katika maeneo yenu,” amesema Chatanda

Aidha Chatanda amesesisitiza kuwa mafunzo hayo pia yatawajenga watendaji na viongozi hao kushauri Chama katika vikao vya kupanga maendeleo katika maeneo yenye uhitaji.

“Haya mafunzo yataendelea hadi kwa madiwani mpaka kwa wabunge ili kuwaimarisha utendajikazi wao katika kuelekea kwenye chaguzi,” amefafanua

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwegelo,amesema  ushirikiano wa kutosha unahitaji miongoni mwa watendaji hao katika kukiwezesha Chama kupata ushindi wa uhakika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji utakaofanyika mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“Kama mnavyofahamu kutokuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2025, katika chaguzi hizo ili tupate ushindi wa kishindo ni muhimu kuwapatia mafunzo yatayowawezesha mshiriki ipasavyo,” amesema Mwegelo

Hata hivyo Jokate ameshukuru  uongozi wa UWT katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kilimanjaro, Kigoma, Kagera, Mbeya, Katavi,Geita na Ofisi ya UWT Zanzibar kwa michango yao kusaidia wananchi waliokumbwa na maafa katika Mji wa Katesh, wilayani Hanang’ mkoani Manyara.

About the author

mzalendo