Featured Kimataifa

RAIS DK.MWINYI ATETA NA WAZIRI WA MAWASILIANO QATAR

Written by mzalendo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Qatar, Mhe. Mohammed bin Ali  Al Mannai na ujumbe wake kando ya ukumbi wa mkutano Hoteli ya Sheraton Grand Doha, Qatar leo tarehe: 11 Desemba 2023.

Katika mazungumzo yao wamegusia ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari ikiwemo masuala yanayohusu uchumi wa kidijitali kwa maeneo watakayokubaliana kupitia mkataba wa makubaliano (MOU)  ambao utaleta mageuzi ya mifumo ya kidijitali utakaoshirikisha Serikali ya Qatar na Tanzania.

Katika kikao hicho wamezungumzia mifumo ya kodi kwa njia za kidijitali kupitia sekta ya Utalii, Huduma za Afya na mapambano dhidi ya rushwa. 

About the author

mzalendo