Featured Kitaifa

NAIBU WAZIRI MKUU ATOA HESHIMA ZA MWISHO MSIBA WA MAREHEMU BABA ASKOFU ERASTO KWEKA

Written by mzalendo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa Ibada Maalumu ya Kuaga Mwili leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro. Kulia kwake ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akizungumza na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Onaeli Shoo kabla ya Ibada ya Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka katika Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo Desemba 5, 2023.
 Familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka na waombolezaji mbalimbali wakiwa katika Kanisa la Usharika wa Moshi Mjini kabla ya Ibada Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu leo Disemba 5, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Baba Askofu Mstaafu, Dkt. Erasto Kweka, kabla ya Ibada Maalum ya Kuaga Mwili wa Baba Askofu leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko Akiaga Mwili wa Marehemu Baba Askofu Mstaafu Dkt. Erasto Kweka, wakati wa Ibada Maalum ya Kuaga Mwili leo Disemba 5, 2023 Usharika wa Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.

About the author

mzalendo