Featured Kitaifa

MAMA NA MTOTO WAUWA KWA KUKATWA VICHWA ULANGA

Written by mzalendo

Mama mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mwanaisha Mateli (37)na mwanae Baraka Juma Mahita mwenye umri wa miaka 7 wameuawa kikatili usiku wa Novemba 24 mwaka huu huko katika Kijiji cha Mavimba Kata ya Milola wilayani Ulanga huku chanzo cha tukio bado hakijafahamika.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mavimba Salahe Kindoki amesema mtu anayedhaniwa kutekeleza mauaji hayo ni kijana ambaye alikuwa akiishi na familia hiyo kwa ajili ya shughuli za shamba ambapo baada ya tukio hilo hakuonekana.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Wial Wilaya ya Ulanga Dkt. Julius Ningu ameelaani kitendo hicho huku akitoa wito kwa jamii kuacha kukaribisha watu wasio wafahamu kwenye makazi yao

About the author

mzalendo