Featured Michezo

SIMBA SC YAANZA NA SARE LIGI YA MABINGWA AFRIKA UWANJA WA MKAPA

Written by mzalendo
SIMBA SC wameshindwa kuondoka na Pointi tatu baada ya kulazimishwa sare  ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa Kundi B Ligi Mabingwa Afrika mchezo uliopigwa  Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
 Simba SC walianza kupata bao kupitia kwa kiungo Mshambuliaji Saido Ntibanzokiza dakika ya 44 kwa Mkwaju wa Penalti bao lililoipeleka Simba mapumziko wakiwa mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko na wageni walipata bao dakika ya 77 likifungwa na Serge N’guessan Archange Pokou na kuisawazishia ASEC Mimosas.
Mechi nyingine ya Kundi B itafuatia baadaye Saa 4:00 usiku baina ya wenyeji, Wydad Athletic Club na Jwaneng Galaxy ya Botswana Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
Simba SC itateremka tena dimbani Desemba 2 Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana kumenyana na wenyeji, Jwaneng Galaxy wakati ASEC Mimosas watakuwa nyumbani siku hiyo kuwakaribisha Wydad Casablanca Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.

About the author

mzalendo