Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO KWA VYAMA VYA MICHEZO NCHINI

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar

………………..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameagiza Mabaraza ya Michezo kuendelea kuratibu na kufuatilia utendaji wa vyama vya michezo na kuhakikisha vinaendeshwa na kujiendesha kwa manufaa ya taifa. 

Rais Samia amesema serikali inapoweka mazingira mazuri katika sekta ya michezo hutoa hamasa kwa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwekeza katika timu za vijana. 

Rais Samia ametoa agizo hilo leo wakati wa hafla ya chakula cha mchana aliyoiandaa kuwapongeza wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu.

Timu ya Karume Boys imetwaa Kombe la Mashindano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yaliyofanyika nchini Uganda ambapo tangu miaka ya 1990 Zanzibar haijawahi kushinda katika mashindano hayo. 

Vile vile Rais Samia amesema michezo hutoa fursa ya ajira kwa makundi mbalimbali hususan vijana hivyo viongozi hawana budi kuweka mipango endelevu na kuwekeza katika sekta hiyo.

Aidha, Rais Samia ameyataka Mashirikisho ya Soka Tanzania bara na Zanzibar kutumia mapato yanayotokana na viingilio vya mechi kufanya ukarabati wa viwanja badala ya kusubiri matengenezo makubwa ambayo yanaongeza gharama maradufu.

 

Kwa upande mwingine, Rais Samia ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kutoa msukumo mkubwa katika kukuza sekta ya michezo nchini ikiwemo kurudisha ligi ya Muungano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Umri wa miaka 15 (CECAFA U-15) kutoka kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Mohamed Ali Mohamed wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Karume Boys, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Kombe la Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati chini ya Umri wa miaka 15 (CECAFA U-15) mara baada ya kukabidhiwa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Vijana Zanzibar chini ya umri wa miaka 15 (Karume Boys) Mohamed Ali Mohamed wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Karume Boys, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.
[11/25, 4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kipa Bora Gloves kutoka kwa Kipa bora wa Mashindano ya CECAFA U-15 Mahir Abdallah Amour wakati wa hafla ya kuwapongeza Wachezaji na Viongozi wa Timu ya Karume Boys, Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.
Wachezaji wa Timu ya Karume Boys wakicheza muziki wa Taarabu wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika Ikulu Tunguu Zanzibar tarehe 25 Novemba, 2023.

About the author

mzalendo