Featured Kitaifa

WIZARA YA KILIMO YAJA NA MIKAKATI YA KUONGEZA UTOSHELEVU WA CHAKULA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi wa Idara ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Ndg.Nyasebwa Chimagu,akizungumza katika Mkutano wa Mafunzo kwa wadau wa kilimo yaliyoandaliwa na AMDT, Novemba 22,2023 jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe.

 

Na Okuly Julius, Dodoma

 

WIZARA ya Kilimo imeweka mikakati ya kuongeza hali ya utoshelevu wa chakula kutoka asilimia 124 iliyopo sasa hadi kufikia asilimia 130 kama ilivyoeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Akizungumza katika
Mkutano wa Mafunzo kwa wadau wa kilimo yaliyoandaliwa na AMDT, Novemba 22,2023
jijini Dodoma, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Mkurugenzi wa
Idara ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Ndg.Nyasebwa Chimagu amesema kuwa
Muelekeo wa kilimo nchini ni KILIMO BIASHARA hivyo chochote kinachozalishwa
kiwe ndio chakula, ajira na biashara.

 

‘’Baada ya
kujihakikishia kuwa utoshelevu wa chakula nchini ni wa kuridhisha sasa Wizara
ya Kilimo imeweka mikakati ya kuhakikisha kilimo kinakuwa cha tija na inawanufaisha
wananchi wapate kipato,ajira na wapunguze umasikini ndio maana tunashirikiana
na wadau kama AMDT kuhakikisha wakulima wetu wanapata mafunzo ya namna ya
kuzalisha kwa tija na kupata masoko kwa ajili ya mazao yao,’’

 

Na kuongeza
kuwa “lengo letu kama sekta ya kilimo ni kuhakikisha wakulima wetu wanazalisha chakula
cha kutosha na kuilisha dunia na hiyo ndio ahadi yetu kuilisha dunia na kwa
mikakati iliyopo na jinsi hali ya upatikanaji wa chakula ilivyo kwa sasa
naamini tutafanikiwa kuilisha dunia kibiashara”amesema Nyasebwa

 

Nyasebwa
amesema kwa sasa Wizara ya kilimo inaandaa MASTER PLAN ya maegeuzi ya kilimo
nchini  ambayo itakuwa inaitwa  ( TANZANIA AGRICULTURE MASTER PLAN 2050)
ambayo itajumuisha malengo yaliyopo katika AGENDA 10/30 na mpango wa pili wa
maendeleo  unaondelea.

 

Amesema kuwa
wakati serikali ikielekea kuhitimisha Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa 2020 –
2025 ndio mwanzo wa maandalizi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa  mpaka 2050 hivyo nayo Sekta ya Kilimo
inaandaa mpango wao ambao utasomana na mpango wa nchi katika sekta zote.

 

 

“tumekuwa
tukiandaa mikakati karibia kila mwaka ila haitekelezwi hivyo malengo ya Sekta
ya kilimo ni kuona sasa inaanza kutekeleza mikakati yote na kuhakikisha
changamoto zilizopo katika sekta hii zinatatuliwa,”

 

Na kuongeza
kuwa “niwaombe wadau wa sekta ya kilimo ikiweo AMDT kuchangia maoni na
mapendekezo katika MASTER PLANI YA KILIMO ili kuhakikisha vikwazo vyote
vinaondolewa na wakulima wakanufaike na kilimo na wajiajiri wapate kipato na
kupunguza umasikini,”ameeleza Nyasebwa

 

Amesema moja
ya changamoto inayokwamisha upatikanaji wa masoko ya uhakika nje ya nchi ni
kukosekana kwa tija hii inasababishwa na kutokidhi viwango vinavyotakiwa
kuanzia kweye ubora,wingi,mabadiliko ya bei sokoni na kuhakikisha kuwa muda
wote tunasambaza bidhaa masokoni.

 

Naye Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini wa AMDT Dk.Mary Shetto alisema wanashukuru ushirikiano
wanaopata kutoka wizara kilimo katika miradi wanayotekeleza katika maeneo
mbalimbali.

 

Alisema  ushirikiano huo umesaidia AMDT kufikia wadau
wengi na kwa usahihi zaidi.

 

“AMDT
imeendelea kushirikiana na wizara katika kupanga mikakati wa nazao mbalimbali
tunaahidi kuwa tutaendelea kushirikiana ili kuhakikisha tunafikia lengo
tulilojiwekea,”alisema

 

Awali
akizungumza katika Mafunzo hayo kwa wadau wa kilimo, Mratibu wa Mradi wa
kujenga kesho Bora (BBT)  Ray Mark amezungumzia
utaratiu wa vijana wanaotekeleza mradi huo kupelekwa kwenye mafunzo maalum ya
Ukakamavu na Uzalendokweny Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Ili wasiyatelekeze mashamba watakayopewa bali
wyathamini na kuyatunza.

 

Mark ametoa
kauli hiyo baada ya mdau wa kilimo kutoka Taasisi ya Farm Afrika, Meshack
Panga  kuhoji ulazima wa vijana hao
kupelekwa JKT na kuwaacha wakulima wengine wakifanya shughuli za kilimo bila
mafunzo ya uzalendo.

 

Panga
amesema kama ni suala la uzalendo kila mkulima apelekwe JKT ili kujifunza
uzalendo na siyo vijana wanaotekeleza mradi wa BBT peke yake.

 

“Kama
ni suala la uzalendo mbona wakulima wengine hawapelekwi JKT, basi na wao
wapelekwe ili kujifunza huo uzalendo,” amesema Panga.

 

Akijibu hoja
hiyo Mark amesema vijana hao wanapelekwa JKT kwa sababu mashamba hayo
hawajayagharamikia bali wamepewa bure tofauti na wakulima wengine ambao
wanamiliki mashamba kwa nguvu zao.

 

Amesema
vijana hao hawana uchungu na mashamba hayokwa sababu hawajatumia nguvu zozote
kutapata hivyo wakiachwanbila kupewa mafunzo ya uzalendo wanaweza kuyatelekeza
tofauti na wakulima wengine.

 

“Hata
ukiangalia watu wenye vitu vya urithi huwa hawana uchungu navyo wanaweza
kurithishwa lakini mwisho wa siku wasivithamini wakaviuza kwa sababu hawajui
thamani yake,” amesema Mark.

 

Amesema
mafunzo hayo ni sehemu ya kuwafanya vijana hao waone mashamba hayo ni mali yao
na si ya mtu mwingine hivyo wan wajibu wa kuyatunza na kuyalima maisha yao
yote.

 

Mratibu huyo
amesema vijana hao watapewa vyumba kwenye maeneo ya mradi ili waweze
kuyasimamia mashamba yao lengo ni kuhakikisha hakuna shamba linalotelekezwa kwa
sababu zozote zile.

 

Amesema
baada ya vijana hao kumaliza mafunzo ya ukakamavu na uzalendo kutoka JKT ndipo
watakapokabidhiwa mashamba hayo kwa ajili ya kuendeleza kilimo ambapo baadhi ya
wadau wameshajitikeza na kupendekeza aina za mazao kwa ajili ya malighafi za
viwanda vyao.

 

Naye Meneja
wa mikopo kutoka benki ya CRDB Kanda ya kati, Sarah Mabula amewataka vijana hao
kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopesheka na kuongeza mitaji kwenye
uzalishaji wa mazao watakayolima kwa sababu benki hiyo inakopesha wakulima
walioko kwenye vikundi peke yake.

 

Amesema
wakulima wanaokopesheka ni wale ambao mashamba yao yanatambuliwa kisheria kwani
wakulima wengi mashamba yao hayajarasimishwa bali wanamiliki kimila hivyo
wakijiunga kwenye vikundi inakuwa rahisi kwao kutambulika na kukopesheka.

 About the author

mzalendoeditor