Featured Kitaifa

RC ARUSHA ATEMBELEA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KITAIFA

Written by mzalendo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela (katikati), akiwasili katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha yanapofanyika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”. Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza, akielezea kuhusu mpangilio wa washiriki katika maadhimisho hayo. 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongela (kulia), akitambulishwa kwa watumishi wa Idara ya Sera, na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Janeth Hiza (katikati), alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Kushoto ni Mchumi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bi. Mwanaidi Kanyawanah.
Mchumi Mkuu kutoka Idara ya Ubia kati ya Sekta Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha, Bw. Enock Kivelege, akitoa elimu kuhusu idara hiyo kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Arusha walipotembelea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. 
Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu ya fedha kwa wananchi mbalimbali waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Afisa Tehama kutoka Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha, Bw. Omary Waziri, akimweleza Mkazi wa Arusha, Bw. Ahmedi Athumani namna ya kutumia Mfumo wa Ukusanyaji Maduhuli ya Serikali (GePG), alipotembelea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mchumi kutoka Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bi. Happy Mwashitete (kushoto), Bi. Diana Mbungu, akitoa elimu kuhusu Usimamizi wa Madeni nchini kwa Mkazi wa Arusha, Bw. Ndetiyo John, alipotembelea katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayoendelea katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)

About the author

mzalendo