Featured Kitaifa

MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA KUWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA FEDHA KARIBU

Written by mzalendo

Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Janeth Hiza (kushoto), akitoa elimu kwa mwananchi wa Arusha, Bw. Stanley Mwami, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Mchumi kutoka Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bi. Happy Mwashitete (kushoto), akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Olasiti, walipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Afisa Usimamizi wa Fedha Mkuu, kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. Abdul Dachi (Katikati), akitoa elimu kuhusu sera mbalimbali zinazotengenezwa na idara hiyo, kwa mkazi wa Arusha, Bi. Magreth Msengi (Kulia), wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Afisa Tehama Mkuu kutoka Idara ya Usimamizi Mifumo ya Fedha, Bi. Tatu Mikidadi (kushoto), akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Olasiti, kuhusu matumizi ya GePG App katika kufanya manunuzi ya Luku, pindi walipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo, akitoa elimu kuhusu namna bora ya kutunza fedha kwa wananchi mbalimbali waliotembelea banda la Wizara ya Fedha wakati wa maadhimisho ya tatu ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, yenye kauli mbiu ya “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi”, yanayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)

About the author

mzalendo