Featured Kitaifa

WANANCHI ILEMELA WASIMAMISHA MSAFARA WA MAKONDA KUMPA PONGEZI ZA RAIS SAMIA NA KUSIKILIZA KERO ZA STENDI YA NYAMONGORO

Written by mzalendo

Wananchi, Wafanya biashara na Wadau mbalimbali Wilayani Ilemela wamesimamisha msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Cde. Paul Makonda kwa kumtaka kumpa salamu zao za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utendaji kazi wake uliotukuka katika kutekeleza miradi mbalimbali Wilayani humo.

” Tunaendelea kumshukuru Rais Samia hakika ni Mama yetu kwani hakuna Mama anayeweza kumuacha mwanae, Mwanza tunaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo tunaomba umfikishie salamu zetu, pia tunakushukuru kwa kukuleta wewe , zamani nilikuwa nimezoea kukuita Mkuu wa Mkoa lakini kwasasa naomba nikuite Mkombozi wa Chama, Msaidie Rais wetu sababu wapo baadhi ya Viongozi hawafanyi kazi ni kama wamelala tuu ” Alisema mmoja katika wafanyabiashara wa stendi hiyo ya Nyamongoro.

Mbali na hilo, wametoa kero na changamoto zao mbalimbali zinazowakumba katika ufanyaji wa shughuli zao za kiuchumi katika stendi hiyo ya Nyamongoro.

Mwenezi Makonda alikuwa njiani kutekea Mwanza kuelekea Mkoani Simiyu katika muendelezo wa Ziara yake, leo tarehe 13 Novemba, 2023.

About the author

mzalendo