Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA MKUU WA WILAYA NA MBUNGE MSTAAFU RUANGWA

Written by mzalendo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 12, 2023, Amewasili Mkoani Lindi ambapo ameshiriki msiba na maziko ya Bi. Fatma Mikidadi aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa nyakati tofauti.

Mheshimiwa Majaliwa amesema Bi. Fatma ni miongoni mwa viongozi wa awali wa Wilaya ya Ruangwa ambao wameacha alama kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Amesema enzi za uhai wake alikuwa miongoni mwa watu waliofanya jitihada kubwa ya kuhakikisha Mkoa wa Lindi unapata maendeleo kwa kushiriki katika miradi ya kuwainua wananchi.

About the author

mzalendo