Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndg. Paul Makonda ametembelea na kukagua mwendelezo wa Ujenzi wa Daraja la JPM (Kigogo – Busisi) lenye urefu wa Kilomita 3 na Barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 1.66 linalojengwa Wilayani Misungwi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa amemueleza Mwenezi Makonda kuwa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia 80% na mpango wa Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia mwezi Agosti mwakani 2024 ujenzi utakuwa umekamilika kwa 100%.
Mwenezi Makonda ameitaka Serikali kuhakikisha inaongeza kasi katika utekelezaji wa Mradi huo.
12 Novemba, 2023
#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#TunaendaNaMama