Featured Kitaifa

MAAGIZO 3 YA CCM NDANI YA SENGEREMA – MWENEZI MAKONDA

Written by mzalendo

Katibu wa Halmashauri Kuu , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda ametoa maagizo matatu ya Chama Chama Mapinduzi mara baada ya kusiliza kero za Wananchi wa Sengerema akiwa njiani kupokelewa katika Jiji la Mwanza ambapo yupo kwa muendelezo wa ziara yake.

Maagizo hayo ni;
1 Chama Cha Mapinduzi kimetoa muda wa wiki moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla kuhakikisha Hospitali ya Wilaya ya Sengerema inafunguliwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

2 Chama Cha Mapinduzi yamuelekeza Afisa Ardhi kuhakikksha hadi kufikia kesho tarehe 13 Novemba, 2023 hati itolewe na ujenzi wa stendi uanze.

3 Aidha CCM yamuelekeza Mkurugenzi wa Halmaahauri ya Sengerema hadi kufikia kesho tarehe 12 Novemba, 2023 Stendi ya Mwembe yanga iliyokuwa imefungwa ifunguliwe kwani ni moja ya malalamiko makubwa ya Wananchi wa eneo hilo.

Cde. Paul Makonda
Katibu wa NEC – Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa.

AKizunguma njiani na Wananchi wa Sengerema Jijini Mwanza kwenye ziara yake leo tarehe 12 Novemba, 2023.

#CCMKazini
#VitendoVinaSauti
#KaziIendelee

About the author

mzalendo