Featured Kitaifa

ANAYEMPINGA SAMIA, ANAMPINGA MAGUFULI KWA MAANA YEYE NDIYE ALIYEMWAMINI SAMIA NA KUWA MAKAMU WAKE WA URAIS – MWENEZI MAKONDA

Written by mzalendo

“Ndugu zangu wa kanda ya ziwa tulipata bahati ya kuwa na Mwasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, tukapata bahati tena ya kuwa na Rais wa awamu ya 5 Hayati John Magufuli ambaye alifanya jambo la kuamini Wanawake wana uwezo na akavunja miiko ya Mwanamke kutokuwa Kiongozi kutokana na Mila na Desturi zetu baadhi akampa Samia kuwa Kiongozi mkubwa na wa kwanza katika histori ya Nchi yetu katika nafasi ya Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akaongeza Wanawake wengi kwenye Baraza la Mawaziri akina Waziri Ummy, Mama Gwajima , Ndalichako na wengine wengi tu”

“Sasa niwaambie ukweli tena kwa dhati ya moyo wangu, kabda ya ziwa atakayempinga Samia ni amempinga Magufuli sababu yeye ndiye aliyemwanini tena kwa vipindi vyote viwili na nakumbuka katika hotuba yake mojawapo Marehemu Magufuli aliwahi kusema kuwa “Nilikuwa sijamfahamu Samia kumbe ni Jasiri, Shupavu na Mchapakazi na akasema alimuamini sana” na ndio maana tunamuona Rais Samia ameendelea kuchapa kazi hakuna mradi uliosimama mikoa yote kanda ya ziwa na Taifa kwa ujumla wake.

Ameyasema hayo leo tarehe 11 Novemba, 2023 wakati alipozungumza na Wananchi wa Wilaya ya Geita akiwa ziarani kikazi katika Mkoa wa Geita

About the author

mzalendo