Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange,akizungumza leo Novemba 1,2023 wakati akizindua Kampeni ya Tumewasikia, iliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange,akizungumza leo Novemba 1,2023 wakati akizindua Kampeni ya Tumewasikia, iliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Mobhare Matinyi,akielezea lengo la Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari hafla iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia ambayo inawataka wakuu wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri nchini, kuandaa mikutano na vyombo vya habari iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, John Kayombo,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dkt. Semistatus Mashimba,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt. Omary Nkullo,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bi. Siwema Hamoud Jumaa,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi Zaina Mlawa ,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Shabani Millao,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kondoa Ndg. Paul Sweya,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi Ally,akielezea mafanikio ya halmashauri hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Tumewasikia Tumewafikia iliyofanyika leo Novemba 1,2023 jijini Dodoma.
Angela Msimbira OR- TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Festo Dugange amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa wananchi unakuwa endelevu na si kusubiri kampeni au tukio maalum.
Dkt. Dugange ametoa wito huo leo Novemba 1,2023 wakati akizindua Kampeni ya Tumewasikia, iliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
‘Wizara inawasisitiza Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakuwa endelevu,’ amesisitiza Dkt. Dugange
Amesema Serikali inataka kuona Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na wataalam wote wa Serikali wanatoa taarifa kwa wakati ili wananchi wajue hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwaboreshea huduma.
Ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa,Dkt. Dugange amewataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa ushirikiano kwa msemaji Mkuu wa Serikali kila atakapohitaji taarifa za kuuhabarisha umma.
Dkt. Dugange amewataka viongozi hao kuwashirikisha katika matukio na kuwapa ushirikiano maafisa habari waliopo katika maeneo yao ili waweze kutekeleza jukumu la kuuhabarisha umma kwa ufanisi.
Ili kuboresha utendaji kazi, Dkt. Dugange amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawana maafisa habari kuhakikisha wanaaajiri maafisa hao kwa mikataba wakati wanasubiri Serikali ikamilishe taratibu za kuwaajiri.