Featured Kitaifa

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

Written by mzalendo

Dar es Salaam
Shirika la Masoko ya Kariakoo linaufahamisha umma na wafanyabiashara kuwa mradi wa ujenzi na ukarabati wa Soko la Kariakoo bado unaendelea na hakuna eneo la biashara lililopangishwa kwa mfanyabiashara yeyote hadi sasa.

Kwa taarifa hii, Shirika linakanusha taarifa zisizo rasmi zinazosambaa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa tayari Soko la Kariakoo limeanza kupangisha maeneo ya biashara.

Taarifa rasmi kuhusu upangishaji wa maeneo yote ya biashara katika Soko la Kariakoo zitatolewa na Uongozi wa Shirika baada ya mradi kukamilika.
Imetolewa na:

Sigsibert K. Valentine
KAIMU MENEJA MKUU

About the author

mzalendo