Featured Kitaifa

MZUMBE NA eGA WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO

Written by mzalendoeditor

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania, CPA Salum Mussa (wapili Kushoto) (kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao), wakiwa wameshika hati za Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA) mara baada ya kusaini.  Wengine katika picha ni Mwanasheria kutoka Chuo Kikuu Mzumbe na Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao.

……………

Chuo Kikuu Mzumbe kimesaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA) kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma za Kitaaluma na Teknolojia zinazotolewa na

Akizungumza wakati wa zoezi la kusaini makubaliano hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha ameeleza kuwa sehemu ya Mpango Mkakati wa Chuo ni kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuongeza wataalamu katika kutoa huduma za kitaaluma ili kuongeza idadi ya wanafunzi na kukuza ufanisi wa programu zinazotolewa na Chuo. Hivyo makubaliano hayo yatasaidia kubadilishana uzoefu na ujuzi kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA).

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi la kusaini mkata huo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Eliza Mwakasangula, amesema makubaliano hayo ni matokeo ya Mkutano wa tatu wa TEHAMA uliofanyika Jijini Arusha kuanzia Februari 8 -12, 2023 ukiratibiwa na eGA.

“Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe umeona fursa na kupitia mradi wa Elimu ya Juu Kwa Mageuzi ya Kiuchumi upande wa Kujenga Ushirikiano wa Kazi na Sekta binafsi, Chuo Kikuu Mzumbe kimepata nafasi ya kuingia makubaliano hayo kwa maendeleo ya Taasisi na taifa” Amesisitiza Dkt. Mwakasangula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali Mtandao, CPA Salum Mussa, amekishukuru na kukipongeza Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua ya kuboresha na kuimarisha mashirikiano na kuwa miongoni mwa Taasisi za elimu ya Juu zinazoshirikiana na eGA moja kwa moja. Kwa niaba ya uongozi wa eGA CPA Salum Mussa, ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa katika mkataba huo yanafikiwa.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania, CPA Salum Mussa (Kushoto) (kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao), wakikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa zoezi la kusaini Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA). 

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania, CPA Salum Mussa (wapili Kushoto) (kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao), wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA).  Wakwanza kulia ni Wanasheria wa Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Eveline Kweka na kushoto ni Meneja wa Huduma za Sheria katika Mamlaka ya Serikali Mtandao, ACP Raphael Rutaihwa. Makubaliano hayo yamesainiwa leo, Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Uwezeshaji katika Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania, CPA Salum Mussa (wapili Kushoto) (kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao), wakiwa wameshika hati za Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA) mara baada ya kusaini.  Wengine katika picha ni Mwanasheria kutoka Chuo Kikuu Mzumbe na Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi, akitoa neno la shukrani mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaini Makubaliano kuhusu ushirikiano wa Huduma za Kitaaluma na Teknolojia kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mamlaka ya Serikali Mtandao Tanzania (eGA).  Makubaliano hayo yamesainiwa tarehe 17.10.2023 Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro.

About the author

mzalendoeditor