Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YASHAURI WIGO ZAIDI FURSA ZA AJIRA ZA WATANZANIA NJE YA NCHI

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wakala wa Huduma za Ajira, Bungeni leo Oktoba 17, 2023, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Rehema Kipera.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeishauri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Kitengo cha Huduma za Ajira kupanua wigo wa fursa za ajira kwa watanzania nje ya nchi.

Akizungumza leo Oktoba 17, 2023 katika kikao cha kamati hiyo cha kupokea na kujadili utendaji kazi wa kitengo hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq, amesema pamoja na juhudi za serikali kufungua fursa za ajira kuna umuhimu wa kuhamasisha watanzania kuchangamkia fursa za ajira nje ya nchi.

Pia, ameshauri kufanyika kampeni maalum ya kukutana na wakala binafsi wa ajira ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Naye, Waziri wa Nchi wa Ofisi, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameahidi kufanyia kazi maoni ya kamati huku akimshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa hatua ambazo amezichukua za kukuza uwekezaji nchini na kufungua fursa za ajira kwa watanzania.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi, amewahimiza watanzania wanaotaka kufanya kazi nje ya nchi kufuata utaratibu unaotambulika na serikali ili iwe rahisi kusaidiwa wanapopata changamoto.

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema kitengo hicho kimetokana na kufutwa kwa Wakala wa Huduma za Ajira (TaESA) na majukumu yake kuunganishwa chini ya Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi.

Akitoa taarifa kwa kamati, Mkurugenzi wa Kitengo hicho, Joseph Nganga amesema miongoni mwa majukumu ya kitengo ni kuwajengea uwezo wahitimu kushindana kwenye soko la ajira, kujenga mtazamo chanya kuhusu kazi na kukuza maadili yanayohitajika na waajiri.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wakala wa Huduma za Ajira, Bungeni leo Oktoba 17, 2023, Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Rehema Kipera.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye, Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii wakati wa kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa shughuli za Wakala wa Huduma za Ajira (TaESA), leo Oktoba 17, 2023 Bungeni, Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia).

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za Kitengo cha Huduma za Ajira, kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bungeni, Jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akieleza jambo wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Ajira, Bw. Joseph Nganga akiwasilisha taarifa ya utrkelezaji wa shughuli za kitengo hicho kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, leo Oktoba 17, 2023 Bungeni, Jijini Dodoma.

 

Baadhi ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA), Bungeni, Jijini Dodoma.

   

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi naM aendeleo ya Jamii wakitoa maoni na ushauri mara baada ya kupokea taarifa ua utekelezaji wa shughuli za Kitengo cha Huduma za Ajira, Bungeni, Jijini Dodoma, leo Oktoba 17, 2023.

About the author

mzalendoeditor