Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga ,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga ,akisisitiza jambo wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga ,akizungumza wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Mratibu wa Kongamano hilo Dkt. Sempeo Siafu,akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Prof. Michael Ng’umbi ,akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika leo Oktoba 12,2023 Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
……………….
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imekuwa ikitekeleza program na Mipango mbalimbali ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kwa lengo la kuwa na Watanzania walioelimika na wenye uwezo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.
Luoga ametoa kauli hiyo leo Oktoba 12, 2023 wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, ambapo amesema miongoni mwa program hizo ni pamoja na Mpango wa Elimu Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA), Mpango wa Elimu Sekondari kwa Njia Mbadala (AEP), Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Shule (IPOSA).
Program nyingine ni Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu na Jamii (MUKEJA), Uzalishaji Mali (UMALI), Shughuli za Ugani (SU) pamoja na Village Community Bank (VIKOBA).
Aidha Kiongozi huyo ameeleza kuwa Serikali inawatarajia Washiriki na Wadau kuchangia kwa tija mijadala mbalimbali katika Kongamano hilo, ili iweze kuisaidia kuja na afua stahiki zitakazo imarisha utolewaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi.
“Kupitia mijadala hii ya leo tunaweza kupata fursa nzuri ya kuinua kiwango cha kujua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa Vijana na Watu Wazima, wanawake na Wanaume ili nguvu kazi hii iweze kuchangia katika kuinua pato la nchi na mtu mmoja mmoja” Alisema Luoga.
Akizungumzia historia ya Maadhimisho hayo, Luoga amebainisha kuwa tangu mwaka 1961, Tanzania imekuwa ikifanya juhudi mahususi katika kukabiliana na tatizo la kutojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
“Katika mwaka 1970 Mwalimu Julius Nyerere alitumia Elimu ya Watu Wazima kuzindua kampeni mbalimbali, ikiwemo Kisomo Chenye Manufaa (KCM), pamoja na program saidizi za kisomo kama vile Elimu Kwa Wafanyakazi” Alifafanua Luoga.
Nae Mratibu wa Kongamano hilo Dkt. Sempeo Siafu amesema Maadhimisho hayo yaliasisiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) mwaka 1966 ili kuikumbusha Jamii umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima, na kulitambua kama suala la heshima na haki za binadamu.
“Hapa Tanzania tumekuwa tukiadhimisha katika ngazi ya Mkoa au Wilaya kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinazotekeleza program za Elimu ya Watu Wazima” alibainisha Dkt. Siafu.
Dkt. Siafu ameongeza kuwa Wizara ya Elimu imeandaa Miongozo mitano ambayo itasaidia katika utekelezaji wa kuimarisha Ubora wa utolewaji wa Elimu ya Sekondari kwa Njia Mbadala (AEP), Mpango unaolenga kuwapa fursa ya kuendelea na masomo Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi hasa Wasichana waliopata ujauzito.
“Nawaasa wadau kutumia Kongamano hili kuangalia namna ya kuboresha Mazingira ya Ujifunzaji katika program za Kisomo yanayozingatia Ubora, Usawa na Ujumuishwaji wa Makundi yote” Alisema Dkt. Siafu.
Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima 2023 yamelenga kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wadau wote pamoja na kupaza sauti kuhusu umuhimu wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kwa jamii.
Awali akizungimza Mkuu WA Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Prof. Michael Ng’umbi amesema Taasisi inatambua kuwa tangu 1960 mpaka sasa Tanzania ilipo mielekeo imekuwa tofauti kwani pamoja na kuendelea na juhudi za kusoma na kuandika, sasa jamii inatilia mkazo kupambana na Mabadiliko.
“Tuitumie Elimu ya Watu Wazima ili kupambana na Mabadiliko yanayoendelea kilanwakati, na ndio Msingi wa kauli mbiu ya mwaka huu 2023 inayosema “Kukuza Uwezo wa Kusoma na Kuandika kwa Ulimwengu Unaobadilika, Kujenga Misingi ya Jamii Endelevu na yenye Amani”.