Featured Kitaifa

SERIKALI YAWATOA HOFU WAMILIKI  SHULE BINAFSI MABADILIKO YA SERA NA MITAALA  YA ELIMU

Written by mzalendoeditor

 

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza  wakati akifungua kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake kilichofanyika leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akisisitiza jambo  wakati akifungua kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake kilichofanyika leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga,akizungumza  wakati wa  kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake kilichofanyika leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza  wakati wa  kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake kilichofanyika leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake kilichofanyika leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma.

Kamishna wa Elimu  Dkt. Lyabwene Mutahabwa,akizungumza  wakati wa  kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake kilichofanyika leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma.

Na.Bolgas Odilo -DODOMA 

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewatoa hofu wamiliki wa shule zisizo za serikali kuwa utekelezaji wa mabadiliko ya sera na mitaala mipya ya elimu 2023 hayatakuwa ya mkupuo.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 10,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda wakati akifungua kikao cha wamiliki wa shule zisizo za Serikali na Wizara yake.

 Prof.Mkenda amesema serikali inahitaji ushirikiano wao na ipo tayari kusikiliza maoni yao na kwamba mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu ya sera na mitaala utekelezaji wake utakuwa wa awamu.

“Mapendekezo yaliyopo kwenye rasimu elimu ya lazima ni miaka 10 ambayo kwasasa ni miaka saba inajumuisha marudio mengi ambayo inaonekana kuchomoa ule mwaka wa saba ili aendelee na kidato cha kwanza hadi cha nne hapotezi kitu,”amesema.

Aidha Waziri Mkenda amesema  kuwa kwenye rasimu ya mitaala imeondoa marudio ambapo elimu ya msingi ni miaka sita lakini mwanafunzi haruhusiwi kukatisha masomo lazima akae shuleni miaka 10.

Hata hivyo ameeleza  kuwa serikali imefanya maandalizi katika kutekeleza hilo ikiwamo vitabu vya kiada na ziada na kuandaa walimu.

Pia Waziri Mkenda ametoa wito kwa wamiliki hao kuwekeza kwenye shule za amali na serikali ipo tayari kushirikiana nao kuwekeza kwenye eneo hilo.

Waziri Waziri Mkenda amesema kuwa wamiliki wa shule binafsi ni watu muhimu na wanahitajika sana   nchini jambo ambalo limepelekea serikali kupiga hatua katika kufaurisha wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi.

“Labda niseme jambo moja muhimu, nyie ni wadau muhimu sana zamani tulikuwa tunaona mabasi yanapishana kwenda nje ya nchi wanafunzi wanaenda kusoma lakini baada ya mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na kuruhusu watu binafsi kuanza kumiliki shule imeweza kutusaidia pakubwa kwa hilo nawapongeza”,amesisitiza Prof. Mkenda.

Kwa upande wake ,Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga, amesema kikao hicho kinalenga kujadili changamoto zinazowakabili na kutafuta namna ya kuzitatua ili kufanya kazi kwa pamoja na kuleta tija kwa taifa.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, amesema kuwa ofisi yao inao wajibu wa kuwaandaa vyema vijana kwaa kushirikiana na taasisi binafsi kwani huko ndipo wanapopatikana wafanyabiashara wazuri watakao kulisaidia taifa .

Pia amesema suala la malezi na makuzi limekuwa suala mtambuka hivyo wasimamizi wa shule wanapaswa kulisimamia vyema suala hilo na kuangalia namna ya kuwekeza na kuwasaidia vijana maana serikali inawetegemea sana wamiliki hao wa shule katika kuwaanda kwa maisha yajayo.

“Naomba pia muangalie namna ya kufanya pale mnapotoa nafasi za kazi kuweza kutoa na nafasi za walemavu na matarajio kama sisi serikali ni kutengeneza usawa katika kila sekta hapa nchi,”amesema Katambi.

About the author

mzalendoeditor