Featured Kitaifa

WAWEKEZAJI SEKTA BINAFSI WAOMBWA KUWEKEZA KWENYE SHULE ZA MAFUNZO YA AMALI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifunga Mkutano kati ya Wizara hiyo na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda,akizungumza  wakati akifunga Mkutano kati ya Wizara hiyo na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda,akisisitiza jambo wakati akifunga Mkutano kati ya Wizara hiyo na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga,akizungumza wakati  Mkutano kati ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki ya wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda,(hayupo pichani)   wakati akifunga Mkutano kati ya Wizara hiyo na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma.

Kamishna wa Elimu  Dkt. Lyabwene Mutahabwa,akizungumza wakati  Mkutano kati ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia  na Wamiliki wa Shule zisizo za Serikali nchini leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma.

       

WAMILIKI wa Shule zisizo za Serikali nchini wameombwa kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya mafunzo ya amali ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inatarajia kuyatilia mkazo kama mapendekezo ya Rasimu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 toleo la 2023 na mabadiliko ya Mtaala wa Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu yatapitishwa na Mamlaka husika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo Oktoba  10, 2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano kati ya Wizara hiyo na Wamiliki wa Shule hizo.

Prof.Mkenda amesema kuwa, Serikali itajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuona ni kwa jinsi gani watasaidia Sekta Binafsi ambao watapenda kuwekeza katika mkondo wa mafunzo ya amali kwani Serikali pekee haitoweza kuanza kwa kasi kwa sababu lazima kuwe na uwekezaji wa kutosha kwani ni dhahiri kuwa watu wataunyanyapaa mkondo wa mafunzo ya amali kama utaanzishwa bila kuwekeza vya kutosha.

“Kuna baadhi ya Shule za Mafunzo ya Amali zipo, zingine tutazifufua, lakini tutaziongezea zaidi. Tunapenda kuwahamasisha wawekezaji wanaohitaji kuwekeza kwenye sekta binafsi wawekeze kwenye upande wa mafunzo ya amali, nawaomba tushikane mikono kwa pamoja kwani tunawahitaji sana kuwekeza katika mkondo huu.” Amesema Prof. Mkenda.

Vile vile, amewashukuru Wamiliki wa shule mbalimbali nchini pamoja na wadau wa elimu kwa kuwekeza katika ujenzi bora wa shule ambapo wameongeza fursa kwa wazazi kuchagua ni wapi wawapeleke watoto wao kupata elimu bora hapa hapa nchini kwani zamani wengi wao walikuwa wakisafiri hadi nje ya nchi kutafuta shule zilizo bora.

“Rais wetu Samia Suluhu Hassan kati ya vitu ambavyo vinamtambulisha ni kuweka msukumo mkubwa na wepesi wa kufanya biashara na kukuza uwekezaji ivyo, katika kutekeleza maelekezo ya Rais wetu tumeona tuwasikilize ili tufahamu ni nni tunatakiwa kukifanya kuleta wepesi katika uwekezaji na uendeshaji wa shule zetu, nyie sio maadui wala changamoto bali ninyi ni fursa na msaada mkubwa kwa Serikali katika kuimarisha elimu.”

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omari Kipanga amesema kuwa wameyachukua mawasilisho yote yaliyowasilishwa na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi kwani isingekuwa kazi rahisi kujibu kila kilichoelezwa katika mkutano huo.

Amesema kuwa Serikali ni sikivu na imeanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto na kusema kuwa huo ni mwanzo hivyo wamepata sehemu ya kuanzia.

“Huu ni mwanzo tu na sio kikao chetu cha mwisho na ilikuwa ni lazima tupate pa kuanzia ameshazungumza kamisha hapa kwa maelekezo ya Mheshimiwa Waziri na kwavile jambo hili ni mtambuka linahitaji Uratibu na ushirikiano wa Wizara zingine,

Tunawahitaji watu wa Wizara ya fedha tuwe nap hapa,tunawahitaji penginewe watu wa Katiba na sheria tufanye nao kazi tunahitaji watu wa Wizara ya utumishi sababu kuna masuala ya kiutumishi hapa yamezungumzwa hao wote wanhitajika ili tuweze kupata muelekeo ambao ni sahihi,”amesema

Aidha amesema kuwa kupitia mkutano huo wanaanza kutengeneza muelekeo mpya na katika kikao kijacho wataanza na kuzitatua changamoto walizozijadili katika mkutano huo na kuweza kujua ni wapi wamefikia.

Naye  Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema katika kikao hicho wamepokea maoni kutoka kwa wamiliki hao wa shule binafsi na lengo ni kuona ni jinsi gani wanarudisha maadili Kwa watoto .

Wamiliki hao wamesema ufundishwaji wa Somo la dini kuanzia elimu ya awali ndio msingi muhimu wa kujenga maadili Kwa watoto wetu wa sasa.

About the author

mzalendoeditor