Michezo

SIMBA SC YASHINDWA KUTAMBA UGENINI CAFCL

Written by mzalendoeditor
MABINGWA Ngao ya Jamii Tanzania Timu ya Simba SC imeshindwa kutamba ugenini katika mechi ya raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya wenyeji Power Dynamos mchezo uliopigwa uwanja wa  Levy Mwanawasa nchini Zambia.
Mabao ya Simba yamefungwa na kiungo fundi Claotos Chama kwa matokeo hayo Simba SC imejiweka nafsi nzuri ya kutinga hatua ya Makundi mchezo wa marudiano utakaopigwa Tanzania Simba inahitaji sare au ushindi wowote.

About the author

mzalendoeditor