Featured Michezo

YANGA SC YANG’ARA UGENINI CAFCL

Written by mzalendoeditor

MABINGWA wa Soka wa Tanzania,Yanga SC imeanza vyema mechi ya raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baada ya kuifumua mabao 2-0 El Merrikh katika mchezo uliopigwa uwanja wa  wa Kigali Pele nchini Rwanda.

Mabao ya Yanga SC  yamefungwa kipindi cha pili yakifungwa na washambuliaji wake Kennedy Musonda dakika ya 60 na Clement Mzize dakika ya 78.

Kwa ushindi huo Yanga SC wamejiweka nafasi nzuri ya kutinga Makundi Ligi ya Mabingwa Msimu wa 2023/24 huku wakiitaji sare yoyote au ushindi mchezo wa marudiano utakaopigwa Tanzania 

About the author

mzalendoeditor