Featured Michezo

WAZIRI NDUMBARO ATETA NA BALOZI WA URUSI MHE. AVETISYAN

Written by mzalendoeditor

Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan leo Septamba 14, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana kushirikiana katika Sekta ya Utamaduni na Michezo ambapo Mhe. Waziri amemkaribisha Balozi huyo katika Mkoa wa Njombe, Mbeya Wilayani Tukuyu, Kigoma na Mbinga Mkoani Songwe kufanya mashindano ya Baiskeli kama ambayo nchi hiyo inafanya mashindano katika nchi ya Rwanda kwakua Jiografia ya maeneo hayo inafaa kwa mchezo huo.

Kwa upande wake Balozi Mhe. Andrey amesema Urusi inafurahia ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania akieleza kuwa Urusi ina Vyuo Vikuu vinne vinavyofundisha lugha ya Kiswahili na kwamba wapo raia wa Urusi ambao wanazungumza na kujifunza lugha ya Kiswahili.

About the author

mzalendoeditor